Na Zainab Nyamka, Michuzi TV

Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt Hassan Abbas amesema serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Hassan Suluhu imejizatiti katika kuinua wanawake kwenye sekta ya michezo kwa ujumla.

Dkt Abbas amesema  Tamasha la Michezo la Wanawake Tanzania -Tanzanite Festival wanawake wanatakiwa kuamka na kuwakumbusha kuwa wanaweza kupata fursa ya kuiwakilishi nchi Kimataifa.

 Hayo ameyasema wakati wa Kongamano kueleka Tamasha hilo litakalofanyjka Septemba 18 mwaka huu,  Dkt Abbas amesema anaamini kufanyika kwa kongamano hili kutatoa mwongozo wa nini kifanyike kwenye kumuinua mwanamke kimichezo.

Dkt Abbas amesema , wanawake wa Tanzania wana thamani kubwa sana duniani na ndio sababu iliyoepelekea Tamasha hili kuitwa Tanzanite.

“Tamasha hili limeitwa Tanzanite kwa sababu wanawake wa Tanzania nyie ni wa thamani kubwa sana duniani, Tanzanite inapatikana katika Nchi pekee ya Tanzania,”amesema Dkt Abbas.

Aidha, amesema kuna baadhi vyama vya michezo vinasema hawapati wadhamini kwenye michezo yao ila kupitia Kongamano hili watatoka na jibu moja namna ya kufanya ili kuhakikisha michezo ya wakina mama inapata fursa  kwa ukubwa wake.

Ameongezea kuwa, katika Kongamano hilo kutakuwa na mada mbalimbali zitakazojadiliwa ikiwemo hali ya ushiriki wa wanawake katika michezo, taaluma na maadili ya wanawake katika kushiriki michezo na umuhimu wa vyombo vya habari, Udhamini katika ukuaji wa soko la michezo ya wanawake Nchini.

Kilele cha Tamasha la Tanzanite linatarajia kuhitimishwa  Septemba 18 kwa michezo mbalimbali kuchezwa kama vile Rede, michezo ya jadi, Karate, Kuvuta Kamba, Kukuna nazi, Mpira wa kikapu kwa walemavu, Kuruka Kamba na mingineyo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt Hassan Abbas

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...