Na. Pamela Mollel, Arusha


Wanawake kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini wamekutana kwa muda wa siku tatu kujifunza matumizi sahihi ya mitandao ili kuepuka madhara mbalimbali wanayoweza kuyapata ikiwemo udhalilishaji.

Mafunzo hayo ambayo yamefanyika jijini Arusha kwa ushirikiano wa vijana wawili Rebecca Ryakitimbo kutoka Kuza Steam Generation na Boniface Witaba kutoka Center for Youth Empowerment and Leardership yalishirikisha vijana wa kike zaidi ya 40 moja kwa moja na wengine kupitia mitandao (Zoom)

"Tuliona hitaji la kuwafunza wanawake hususan vijana kufahamu utawala wa kimtandao na sera kwa kuanzisha mradi wa kuelimisha wanawake kuhusu masuala ya kimtandao (ARUWSIG) ili kuziba pengo kubwa la kidijitali lililopo nchini kote" alisema Waitaba na kuongeza kuwa,

Takwimu zinaonyesha karibu 50% ya vijana wanatamani kufanya jambo lenye manufaa kwenye mtandao lakini hawana maarifa na taarifa sahihi za pakuanzia hivyo wakaona kuna haja ya kutoa mafunzo hayo kwa kinadada ili wapate manufaa chanya ya mtandao.

Kwa upande wa Rebecca Ryakitimbo alisema mafunzo wanayoyatoa ni yale ya ulinzi wa mitandao, Sheria zinazowalinda, kubadili maudhui ya mitandao kwa lugha ya kiswahili ili waweze kuelewa kwa urahisi, kuwezesha wanawake kujifunza lugha kupitia kirekebisha matamshi (Common Voice) lakini pia kusaidia wanawake kutambua fursa mbalimbali zilizopo mitandaoni.

Piter Mbando msimamizi wa warsha alisema limeibuka wimbi la wezi mitandaoni ambao wanasambaza "link" mbalimbali ambazo zinawashawishi watumiaji wa mitandao kuweka namba zao za simu, E-mail zao na hata akaunti za benki jambo linalo wapelekea kuibiwa.

"Washiriki wamejifunza namna ya kujilinda kwenye mitandao, kuona fursa kwenye mitandao ili wanufaike, kutambua link zipi ni sahihi na zipi ni matapeli, namna ya kufanya kazi kwa ufanisi kupitia mitandao bila ya kufika ofisini hasa katika kipindi hiki cha UVIKO 19 na tahadhari ya kutowaamini mafundi simu kwa kuwapa taarifa zao simu zinapo haribika" aliongeza

Katika kuhakikisha elimu hiyo inawafikia vijana hao wa kike taasisi zinazo husika na maudhui ya kimtandao walishiriki kutoa mada mbalimbali ikiwemo "Mozilla" walitoa mafunzo ya namna ya kutamka maneno kwa usahihi huku taasisi kama Localization lab, Article 19, Paradigm Initiative, ICANN na Facebook waliwezesha kutolewa mada mbalimbali.

Kwa upande wake mshiriki wa mafunzo kutoka Dodoma Vanessa Amada alisema amejifunza namna ya kujilinda anapotumia mitandao ya kijamii lakini pia jinsi ya kutumia mitandao ya kijamii ili kujikuza kiuchumi.

"Kwa mfano mimi nipo sekta ya afya na tumejifunza namna mitandao inavyochangia mtu kuwa na afya ya akili iliyo sawasawa au yenye tatizo hivyo mbali na matibabu ya kawaida nitakuwa nashauri nitakao watibu kutumia mitandao vizuri" alisema.

Naye Fatma Cherepa mshiriki kutoka Dar Es Salam alisema hivi sasa anatambua namna ya kujilinda na kuwalinda wanawake kwenye mitandao.

"Wanawake wengi hawafahamu haki zao za kimtandao na wamekuwa wahanga wa kuvujishwa picha zao kwenye mitandao huku hawajui pakuanzia" alifafanua.

Hata hivyo warsha hiyo ni ya nne kufanyika tangu kuanzishwa kwake ambapo wanawake zaidi ya 300 wameweza kupata mafunzo ya moja kwa moja mbali na wale waliojifunza kupitia waliopata mafunzo.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya matumizi bora ya mitandao wakisikiliza mada mbalimbali, mafunzo hayo yaliyofanyika jijini Arusha yaliwajumuisha kutoka mikoa mbalimbali mbalimbali hapa nchini.(Picha na Pamela Mollel).

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...