Raisa Said,Kilindi
Serikali imeombwa kuangalia uwezekano wa kuongeza vyanzo vingine vya mapato kwaajili ya bajeti za lishe badala ya kusubiri chanzo kimoja cha mapato ya ndani ya Halmshauri husika.
Ombi hilo limetolewa na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kilindi Dk Daniel Chochole wakati Akizungumza na Mwandishi wa Habari hizi kuhusu hali ya lishe katika Wilaya hiyo.
Dk Chochote alisema kuwa endapo Serikali itaongeza vyanzo hivyo vya mapato vitasaidia katika kutekeleza afua mbalimbali za lishe ili waweze kutengeneza afya bora za watoto wenye umri chini ya miaka mitano katika makuzi yao.
Mganga Mkuu huyo alisema kuwa kumekuwa na changamoto Katika utekelezaji was afua mbalimbali za lishe kutokana na kutegemea Makusanyo kutoka katika vyanzo vya halmshauri.
" kwasasa tumekuwa tukitumia bajeti za lishe kutoka katika vyanzo vya mapato vya halmashari"Alisema Dr Chochole nakuongeza kuwa Makusanyo ya Halmshauri kwa miaka hii miwili yamekuwa madogo hivyo kumesabisha changamoto Katika utekelezaji wa afua mbalimbali za lishe.
Kwa upande wake Kaimu Mratibu wa Lishe wilani Kilindi Fikiri Adam alieleza kuwa kwa mwaka huu wa fedha wa 2020/2021 serikali imewatengea kiasi cha milion 40 kwa ajili ya utekelezaji wa afua mbalimbali za lishe wilayani humo.
Adamu alisema kuwa kwasasa wanaendelea na utekelezaji ikiwemo kutoa elimu mbalimbali ihusuyo namna Bora ya uaandaji wa lishe bora kwa mtoto ili kumuandaa makuzi yao ya Kila siku.
Hata hiyo lishe bora na huduma zingine za msingi kama elimu na afya ni haki ya kila mtoto kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, lakini mara nyingi mamilioni ya watoto hukosa haki hiyo hususani lishe bora kutokana na sababu mbalimbali. UNICEF inasema hali hiyo inaweka afya za watoto hatarini na pia njiapanda mustakhbali wao.
Home
HABARI
SERIKALI YAOMBWA KUANGALIA UWEZEKANO WA KUONGEZA VYANZO VINGINE VYA MAPATO KWA AJILI YA BAJETI YA LISHE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...