Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka amesema hakuna ahadi iliyotolewa kwenye ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020-2025 ambayo haitatekelezwa ikiwemo mpango wa elimu bila malipo na utatuzi wa changamoto za sekta ya elimu nchini.

Amesema hayo wakati akikagua Ujenzi wa shule ya sekondari ya wavulana Nachingwea iliyopo kata ya Chiumbati mkoani Lindi.

 "Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan itaendelea kugharamaia elimu bila malipo. Ikiwa ni utekelezaji wa waraka wa elimu namba 6 wa mwaka 2015 na ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025" Alisema Shaka

Aliwataka wananchi wapuuze taarifa zozote za upotoshaji zinazodai serikali itasitisha mpango wa kugharamia elimu bila malipo.

 "Serikali ya CCM inayoongozwa na Rais Samia imeendelea kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya elimu ikiwemo kuajiri walimu takribani 6,949 na katika bajeti ya 2021/22 imetenga kiasi cha fedha shilingi bilioni 125 za kukamilisha maboma elfu kumi nchi nzima ikiwa ni utekel
ezaji wa ibara ya 80 ya ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025." Alifahamisha Shaka.

Shaka amewapongeza wananchi wa kata ya Chiumbati, kijiji cha Chiumbati shuleni kwa kutoa eneo la ujenzi wa shule hiyo, kujitolea nguvu kazi na hata kuchangia ujenzi katika hatua za awali kabla ya serikali kuwaunga mkono kuendeleza ujenzi huo.

Hata hivyo  Wananchi wa eneo hilo wamemshukuru Rais Samia katika kuipa kipaumbele elimu na kufanikisha hatua za ujenzi wa shule hiyo ya wavulana  ambayo ilikuwa ni hitaji lao la muda mrefu.

Shaka pia amewataka wananchi kujitokeza kushiriki kikamilifu katika zoezi la sensa ya watu na makazi itakayofanyika mwaka 2022. Alihimiza serikali inatekeleza zoezi hilo kwani taarifa zake zina umuhimu mkubwa katika kuisaidia serikali kupanga rasilimali zake katika maendeleo ya nchi na watu wake hivyo ni muhimu kila mmoja kujitokeza kulishiriki.

Shaka yupo kwenye ziara ya Sekretarieti ya CCM Taifa inayokamilika leo mkoani Lindi ikiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...