Na Zainab Nyamka, Michuzi TV
BODI ya Ligi (TPLB) imetangaza ratiba ya Ligi Kuu Tanzanua Bara itakayoanza kutimua vumbi Septemba 27 mwaka huu.
Bodi ya Ligi wameweka wazi ratiba hiyo ambapo watani wa jadi Simba na Yanga Zitakutana tena Desemba 11 ukiwa ni mchezo wa tano ndani ya mwaka mmoja.
Timu hizo tayari zimekutana mara tatu na zinatarajia kucheza kwenye mchezo wa Ngao ya Hisani Septemba 25 ukiwa ni mchezo wa nne ndani ya mwaka mmoja.
Yanga na Simba zimekutana kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la Mapinduzi ambapo Yanga walifanikiwa kushinda kwa mikwaju ya penati, wakakutana tena kwenye mchezo wa ligi kuu Yanga ikiibuka kwa ushindi wa goli 1-0.
Mchezo wa tatu ulikua ni wa Fainali ya Kombe la Azam, Simba waliibuka kidedea kwa kushinda Na kuqa mabingwa wa kombe hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...