Na Jamaly Mussa, DSJ

STAA  wa muziki nchini Nigeria Korede Bello aliyetambulishwa katika tasnia ya muziki na msanii na kiongozi wa wasanii kataka lebo ya Mavin Records mwaka 2014 ameweka rekodi ya kuuza nakala zaidi ya 500,000 nchini Marekani kwa njia ya mauzo ya muziki unaofanyika mitandaoni.

Rekodi hiyo ameiweka kupitia wimbo wake wa Do Like That ambao ameutoa mwaka 2016 na mwaka huu wimbo huo umetimiza miaka mitano.Hivyo ngoma hiyo  imepewa cheti cha Gold baada ya kufikisha kiwango hicho cha mauzo ya nakala katika njia ya mtandao katika nchi ya Marekani pekee.

Kabla ya hapo tokea kutambulishwa kwake msanii huyo mwaka 2014 aliwahi kutoa kibao kiitwacho Godwin alichokitoa mwaka 2015 na kibao hicho kilifanya vizuri katika chati za muziki barani Afrika pamoja na nchi karibu za ughaibuni.

Staa huyo anaingia kwenye orodha ya mastaa wanaotokea nchini Nigeria waliowahi kufikia kiawango hicho cha mauzo nchini Marekani, wasanii hao ni Wizkid, Davido, Burnaboy. Kwa upande wa Afrika Mashariki hakuna msanii yoyote aliweza kufikisha au kuweka rekodi ya mauzo ya nakala kama hizo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...