Tunaipongeza Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Wizara ya  Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambao walitualika tukafanya vikao  kadhaa na tasnia hii ili kujadili mbinu za haraka na za muda mrefu ili kufanikisha azma ya Serikali ya kuanzisha mchango wa maendeleo ya Jamii (Solidarity Levy) na vile vile kujadili kwa mapana ustawi wa sekta ya mawasiliano.

Pamoja na hayo, tunaipongeza serikali kwa kupunguza 30 asilimia na kutoweka miamala ya bei ya chini katika utekelezaji wa agizo hili. 

Tunatumai hii pamoja na upunguzaji wa 10 asilimia ya ada za miamala kwenye miamala inayofanyika baina ya wateja wa makampuni tofauti zitarudisha wateja ambao waliacha kufanya miamala tangu kuanza kwa utekelezaji wa agizo hili.

Katika enzi hii ya mapinduzi ya nne ya viwanda, sekta inayostawi ya mawasiliano ina jukumu muhimu la kuwezesha sekta zingine kama teknolojia ya kilimo (Agritech), huduma ya matibabu kwa video (telemedicine) na malipo ya serikali na huduma, nikitaja hayo machache, ili kuendelea kuchangia ukuaji wa Taifa. Mpaka  wakati huu, wanachama wa TAMNOA wamejitolea kuendelea kuwekeza katika uvumbuzi mpya, lakini ili kuwezesha hili, lazima tuendelee kubaki na faida.

Kwa hiyo, kwa muda wa kati na mrefu ujao, bado ni muhimu kwa tasnia kufanya kazi kwa karibu na Serikali ili kushirikishana maarifa na njia bora zaidi za jinsi ya kupata majukwaa ya kidijitali yatakayowezesha ukusanyaji wa kodi kwa ukaribu na mamlaka husika na wadau wengine ili kuhakikisha kunakuwa na usawa latika kutimiza matazamio ya jamii yetu.

-Hisham Hendi, Mwenyekiti- TAMNOA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...