Kufanya michoro ya ramani kwa ajili ya nyumba ya ghorofa ni
tofauti sana na kufanya michoro ya ramani kwa nyumba isiyo ya ghorofa,
na utofauti huu haupo kwenye gharama ya michoro ya ramani peke yake bali
pia kuna tofauti kubwa kwenye matokeo ya mwisho.
Kwanza michoro ya ramani kwenye ujenzi wa nyumba ya ghorofa imegawanyika
mara mbili ambapo kuna michoro ya ramani za usanifu wa jengo ambayo
inafanywa msanifu majengo, kisha kuna michoro ya ramani za mihimili ya
jeng ambayo inafanywa na mhandisi mihimili.
Kwa hiyo licha ya kwamba michoro ya ramani za mradi wa nyumba ya ghorofa
ni kubwa zaidi, inayohusisha vitu vingi zaidi na inayohitaji kutumia
akili zaidi kuweza kuleta uwiano kati ya ghorofa ya chini na ghorofa ya
juu lakini pia inahusisha utaalamu mwingine wa uhandisi mihimili.
Hapo tunaona kwamba sasa gharama ya michoro ya ramani kwa nyumba ya
ghorofa inafika angalau mara tatu zaidi ya nyumba ya kawaida kwa sababu
licha ya kwamba changamoto yake ni mara mbili ya nyumba ya kawaida
lakini ukiongezea na gharama ya michoro ya ramani za uhandisi mihimili
gharama yake inaenda angalau mara tatu zaidi ya gharama za michoro ya
nyumba ya kawaida.
Hata hivyo umakini mkubwa sana unahitajika kwenye kutengeneza michoro ya
ramani za nyumba ya ghorofa ili kuhakikisha vipengele vyote vinavyoleta
mvuto wa jengo vinapangiliwa kwa usahihi na pia kanda zote zinazoenda
kimatumizi ndani ya jengo zinapangilia kwa usahihi ili kurahisisha
mzunguko wa watu na vitu ndani ya nyumba husika.
Karibu kwa ushauri wa kitaalamu.
Architect Sebastian Moshi.
Whatsapp/Call +255717452790.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...