TANZANIA ni kati ya nchi ambayo inatumia vema huduma za kidigitali kwenye sekta ya fedha ambapo kwa sasa imekuwa siyo tena mapinduzi tu ya mifumo ya kidigitali bali ni sehemu ya maisha ya kila siku ya huduma za kifedha nchini.
Hayo yamebainishwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni za Letshego Group yenye makao yake makuu nchini Botswana, Andrew Fening katika taarifa yake kwa vyombo vya habari nchini kuhusiana na huduma za kibenki za benki hiyo ambapo ilibainisha kuwa Tanzania inaendana na maendeleo ya kidigitali sekta za Fedha huku akitaka kubuniwa kwa njia sahihi zitakazomwezesha mteja kupata huduma kwa ukaribu, uharaka na urahisi.
Akizungumzia kuhusiana na huduma hiyo, alisema itamwezesha mtumiaji kupata huduma za taarifa mbalimbali za mikopo, kufanya mihalamala na kupata huduma nyingine za kifedha kwa haraka.
Alisema:” kutokana na changamoto kadhaa kama vile ugonjwa wa covid kwa sasa kuna uhitaji wa kuja na mikakati kama hii ya kushughulikia huduma za kibenki kwa njia ya kidigitali ili kuwawezesha wateja kutosongamana wakati wa kupata huduma.
"Kwa sasa wanaweza kupata huduma kwa njia ya simu zao za mkononi au televisheni na tena wakanufaika kwa haraka na ufanisi zaidi huku wakiwa wamejirinda na ndiyo maana Letshego imekuwa karibu zaidi kuwahudumia wateja wake kibunifu.”
Alisema kuwa, benki hiyo itaendelea na utamaduni wake wa kutumia zaidi matumizi ya mifumo ya kidigitali hasa huduma ya LetsGo katika kuwaunganisha wateja wake ili waendelee kufurahia huduma.
Alisema,“Kwa sasa LetsGO platform inaweza kupatikana kupitia simu ya mkononi na tovuti ambapo mteja ataweza moja kwa moja kuingia kwenye akaunti yake na kuendelea kujipatia huduma kama za mikopo, taarifa mbalimbali na huduma nyinginezo kwa Botswana na Nigeria”.
Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa Letshego Tanzania, Andrew Tarimo, alibainisha kuwa muda mfupi ujao wateja wa Taasisi hiyo hapa nchini wataanza kunufaika na ubunifu huo wa kidigitali wa kupitia huduma ya Lets Go ambayo itawaunganisha na wateja wengine Afrika.
“Kwa pamoja tutumie fursa zinazopatikana kwenye huduma hii ya kidigitali ya LetsGo kukua pamoja kwa kuwa ndipo dunia inapoenda na Afrika ya baadaye yenye matumizi bora ya kidigitali inaanza sasa.” alisema Andrew Tarimo.
Walisema kuwa huduma hiyo itaendelea pia kwa nchi nyingine tisa za Afrika huku akibainisha kuwa lengo la huduma hiyo ni kuhakikisha kuwa itatumika kama njia sahihi na salama ya kidigitali kwa taasisi hiyo.
CEO Letshego Bank Tanzania, Andrew Tarimo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...