Kaimu Mkurugenzi Idara ya Fedha Benki ya Exim Bw Issa Rajabu (Kushoto) akikabidhi msaada wa fedha taslimu kwa Muhasibu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKIC) Bw Mohamed Isimbula ikiwa ni mchango wa wafanyakazi wa benki hiyo ili kusaidia matibabu ya moyo kwa mtoto John Selemani (aliebebwa na mama yake) kutoka mkoani Tanga wakati wafanyakazi hao walipomtembelea mtoto huyo hospitali hapo jijini Dar es Salaam leo
Afisa Muuguzi Msimamizi wa wodi ya watoto Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKIC) Bi Theresia Marombe (Kulia) akielezea huduma zinazotolewa na taasisi hiyo kwa wafanyakazi wa benki ya Exim walipomtembelea na kutoa msaada wa fedha kwa mtoto John Selemani anaepatiwa matibabu kwenye kituo hicho.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Fedha Benki ya Exim Bw Issa Rajabu (wa tano kushoto) akitoa la faraja kwa wazazi wa mtoto John Selemani (aliebebwa na mama yake) pamoja na uongozi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKIC) baada ya kukabidhi mchango huo. Wengine ni wafanyakazi wa benki hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...