Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro amezitaka nchi za Afrika kuwa na kauli moja kuhusu taratibu na bei za wanyamapori katika biashara uwindaji wa kiutalii
Ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza kwa nyakati tofauti katika vikao ana kwa ana na baadhi ya mawaziri wa Utalii wa nchi za Afrika katika Mkutano wa 64 wa Kimataifa wa Utalii uliondaliwa na Shirika la Umoja wa Kimataifa la Utalii Duniani (INWTO) unaofanyika kwa muda wa siku nne nchini Cape Verde.
Amesema bei za wanyama wanaoruhusiwa kuwindwa pamoja na vitalu vya uwindaji wa Wanyamapori zimekuwa zikitofautiana sana kati ya nchi na hali hali hiyo imekuwa kikwazo kikubwa kwa shughuli uhifadhi barani Afrika.
Akizungumza katika vikao hivyo vya ana kwa ana na Waziri wa Utalii wa Zimbabwe.Mhe.Ngobhithize Ndlovu amezitaka nchi hizo kuwa kitu kimoja katika kuamua na kupanga bei za uwindaji wa Kitalii.
Amesema kutokana na kutofautiana kwa bei na baadhi ya kanuni na taratibu hizo Wawindaji wa kiitalii wamekuwa wakitumia mwanya huo kuzikandamiza nchi za Kiafrika kwa kupanga bei wanazotaka wao huku wakidai kuwa bei hizo cha chini zimekuwa katika nchi nyingine pia.
Amesema Wawindaji hao wamekuwa wakipanga bei za uwindaji wa kiutalii na sio nchi husika huku wakidai kuwa kama bei hiyo haitawezekana basi watakwenda katika nchi nyingine ambayo utalii wake uwindaji ni bei ya chini zaidi ” Utofauti wetu huu umekuwa ukitukandamiza kama nchi kwani tulitakiwa sisi ndo tupange bei lakini kutokana na kutokuwa na umoja bei za wanyama zimekuwa zimekuwa zikiamuliwa na wao hili lazima tulikatae kwa kuungana kwa pamoja ” alisisitiza Dkt.Ndumbaro
Kufuatia hali hiyo, Dkt.Ndumbaro amezitaka nchi zote zinazoendesha utalii wa uwindaji zifanye mkutano kwa nji ya mtandao ili kujadili mustakabali wa biashara hiyo na kisha zitoke na kauli moja ili kuwathibiti wawindaji wa kitalii kwa ajili ya maslahi mapana ya uhifadhi barani Afrika.
Amezitaja baadhi ya nchi wanachama wa SADC zinazofanya vizuri katika uwindaji wa kitalii kuwa ni Botswana, Zimbabwe pamoja, Zambia na Afrika ya Kusini
Katika hatua nyingine , Dkt.Ndumbaro ametoa ahadi kwa nchi ya Zimbabwe kama itakuwa tayari ipewe mafunzo ya kuendesha biashara ya uwindaji wa kiutalii kwa mfumo wa kidigitali ambao utasaidia kuongeza mapato maradufu
Amesema tangu kuanzisha kwa mfumo huo nchini Tanzania umeleta manufaa makubwa kwa nchi ambapo Wawindaji wa kitalii ili kuweza kupata vitalu vya uwindaji wamekuwa wakilazika kushiriki katika mnada wa kimtandao.
Naye, Waziri waUtalii wa ZimbabweMhe.Ngobhitithize Ndlovu amesema nchi za kiafrika lazima ziungane katika suala hilo kwani katika nchi ya Zimbabwe Wawindaji hao pia wamekuwa wakipanga bei huku wakidai kama hiyo bei haitawezekana watakwenda Tanzania ambako bei vitalu vya uwindaji ipo chini zaidi
Amesisitiza kuwa shughuli za uhifadhi zimekuwa aghali sana huku biashara hiyo ya uwindaji wa kiutalii ukibaki pale pale kutokana na kutofautiana kutoka nchi moja hadi nyingine
Naye, Kamishna Uhifadhi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Mabula Misungwi amesema umoja huo wa nchi za Kiafrika katika biashara ya vitalu vya uwindaji italiingizia taifa fedha nyingi za kigeni sio kwa Tanzania pekee bali kwa Afrika nzima
” Biashara hiyo imekuwa na ushindani baina yetu bila kujuana kufuatia kila nchi kupanga bei zake kulingana na matakwa ya wadau hao huku shughuli za uhifadhi zikiwa juu zaidi” amesisitiza Kamishna Mabula.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro (wa pili kuli) akiwa kwenye
picha ya pamoja na na Waziri wa Utalii wa Zimbabwe mara baada ya kikao
cha kujadili uwindaji wa kitalii pembeni mwa Mkutano wa Kimataifa wa
64 wa Utalii Kanda ya Afrika ulioandaliwa na Shirika la Umoja wa
Mataifa la Utalii (UNWTO) unaoendelea kufanyika katika kisiwa cha SAL
nchini Cape Verde, Mkutano huo umewakutanisha Mawaziri wa Utalii 30
lengo likiwa ni kujadili mustakabali wa utalii Barani Afrika na Duniani
kwa ujumla.Kulia ni Balozi wa Paris Ufaransa Mhe.Samweli Shekindo pamoja
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii ya Zimbabwe Dnomal dinamo
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro (kuli) akizungumza na
Waziri wa Utalii wa Zimbabwe kuhusiana na kuwa na bei ya pamoja ya
uwindaji wa kitalii katika nchi wanachama wa SADC katika kikao
pembeni katika Mkutano wa Kimataifa wa 64 wa Utalii Kanda ya Afrika
ulioandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii (UNWTO)
unaoendelea kufanyika katika kisiwa cha SAL nchini Cape Verde, Mkutano
huo umewakutanisha Mawaziri wa Utalii 30 lengo likiwa ni kujadili
mustakabali wa utalii Barani Afrika na Duniani kwa ujumla.
Kamishna
Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS) Prof.Dos Santos
Silayo ( wa kwanza kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Utalii,
Philip Chitaunga wakishiriki katika kikao cha ana kwa ana katika ya
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro (kuli) akizungumza na
Waziri wa Utalii wa Zimbabwe kuhusiana na kuwa na bei ya pamoja ya
uwindaji wa kitalii katika nchi wanachama wa SADC katika kikao
pembeni katika Mkutano wa Kimataifa wa 64 wa Utalii Kanda ya Afrika
ulioandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii (UNWTO)
unaoendelea kufanyika katika kisiwa cha SAL nchini Cape Verde, Mkutano
huo umewakutanisha Mawaziri wa Utalii 30 lengo likiwa ni kujadili
mustakabali wa utalii Barani Afrika na Duniani kwa ujumla.
Afisa
Utalii kutoka Bodi ya Taifa yaUtalii ( TTB) Naomi Mbilinyi ( wa pili
kulia) akiwa akifuatilia mada ya kutumia mitandao ya kijamii katika
kutangaza vivutio vya utalii katika Mkutano wa Kimataifa wa 64 wa
Utalii Kanda ya Afrika ulioandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la
Utalii (UNWTO) unaoendelea kufanyika katika kisiwa cha SAL nchini Cape
Verde, Mkutano huo umewakutanisha Mawaziri wa Utalii 30 lengo likiwa ni
kujadili mustakabali wa utalii Barani Afrika na Duniani kwa ujumla.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza na jambo na
Waziri wa Utalii wa Gambia, Mhe. Hamat Bah mara baada ya Mkutano wa
Kimataifa wa 64 wa Utalii Kanda ya Afrika ulioandaliwa na Shirika la
Umoja wa Mataifa la Utalii (UNWTO) unaoendelea kufanyika katika kisiwa
cha SAL nchini Cape Verde, Mkutano huo umewakutanisha Mawaziri wa
Utalii 30 lengo likiwa ni kujadili mustakabali wa utalii Barani Afrika
na Duniani kwa ujumla ambapo wamekubaliana kushirikiana katika kutangza
vivutio vya utalii kwa pamoja kama Bara la Afrika.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza na jambo na
Waziri wa Utalii wa Nigeria, Alhaji Mohammed katika mara baada ya
Mkutano wa Kimataifa wa 64 wa Utalii Kanda ya Afrika ulioandaliwa na
Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii (UNWTO) unaoendelea kufanyika
katika kisiwa cha SAL nchini Cape Verde, Mkutano huo umewakutanisha
Mawaziri wa Utalii 30 lengo likiwa ni kujadili mustakabali wa utalii
Barani Afrika na Duniani kwa ujumla ambapo wamekubaliana kushirikiana
katika kutangza vivutio vya utalii kwa pamoja kama Bara la Afrika.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza na jambo na
Waziri wa Utalii wa Kenya , Mhe. Najib Balala katika mara baada ya
Mkutano wa Kimataifa wa 64 wa Utalii Kanda ya Afrika ulioandaliwa na
Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii (UNWTO) unaoendelea kufanyika
katika kisiwa cha SAL nchini Cape Verde, Mkutano huo umewakutanisha
Mawaziri wa Utalii 30 lengo likiwa ni kujadili mustakabali wa utalii
Barani Afrika na Duniani kwa ujumla ambapo wamekubaliana kushirikiana
katika kutangza vivutio vya utalii kwa pamoja kama Bara la Afrika.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...