Charles James, Michuzi TV

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Ummy Mwalimu ameitaka Tume ya Utumishi wa walimu (TSC) nchini kutoa kibali cha uhamisho kwa mwalimu anayehitaji kuhama kutoka mjini kwenda kijijini kitolewe ndani ya siku Saba.

Kadhalika tume hiyo  imetakiwa kuweka usawa wa idadi ya walimu katika Halmashauri zote za mijini na vijijini ili wanafunzi  wapate haki sawa katika masomo

Waziri Ummy ameyasema hayo Leo September 9 jijini hapa wakati akifungua mkutano wa kwanza wa baraza la wafanyakazi tawi la tume ya Utumishi wa walimu,ambapo amesema pamoja na mambo mengine wahakikishe kwamba wao kama tume  wasimamie masuala ya  uwiano sawa wanapotaka kumuhamisha mwalimu kutoka kijijini kwenda  mjini wahakikishe wamepeleka walimu wengine kabla ya kuwahamisha.

" Mfano utakuta mwalimu anamwenzawake yupo kijijini na anaomba kibali cha kwenda kufanya kazi alipo mwenzawake haina haja ya kuweka mizunguko mingi mpeni kibali aende ndani ya hizo siku saba, " Amesema Waziri Ummy. 

Sambamba na hilo ameipa 14  tume hiyo kutoa takwimu katika kila halmashauri hali za walimu wanaohitajika,waliopo,pamoja na  ameitaka tume hiyo kutoa kibali cha uhamisho cha mwalimu anaetaka kuhama kutoka mjini kwenda kijijini ahamishwe ndani ya siku Saba.

" Niwaombe muendelee kuwapa mafunzo walimu wazingatie maadili yao waachane na uzembe kazini, ulevi, wavae mavazi yenye staha lugha nzuri hata tabia na suala la walimu kujihusisha na mahusiano na wanafunzi hili natoa agizo kali muwachukulie hatua walimu wote wanaohusika na tuhuma hizo haijalishi wakike au wakiume" amesema Ummy.

Pia ameitaka tume hiyo kutumia tehama kwaajili ya kufatilia  mahudhurio  ya walimu  kila wanapoingia kazini kusaini pamoja na wakati wa kutoka.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi Mwalimu Paulina Nkwana amemhakikishia Waziri  kwamba watajitahidi kushughulikia malalamiko ya walimu kwa wakati ambayo yamekuwa yakiwasumbua kwa muda mrefu

"Tunashukuru kwa kutuamini na kama ilivyo asilimia 51 ya watumishi wa umma ni walimu, pia tunampongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kutupandishia madaraja na jumla ya mishahara mpya  ya walimu laki 1,26,349"amesema Mwalimu Nkwana.

" Tukutoe hofu  kwamba baraza linafanya kazi ya kughulikia changamoto  mbalimbali  ikiwemo mafao, kushughulikia masuala ya maadili na mambo mbalimbali  yanayowahusu walimu"amesema.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Ummy Mwalimu akizungumza na viongozi na watumishi wa Tume ya Utumishi ya Walimu leo jijini Dodoma.
Viongozi na Watumishi wa Tume ya Utumishi wa Walimu TSC wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Ummy Mwalimu alipokua akizungumza nao kwenye kikao Cha pamoja leo jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Utumishi wa Walimu TSC, Pauline Nkwana akizungumza mbele ya Waziri wa Tamisemi, Ummy Mwalimu kwenye mkutano baina ya Waziri na na Tume hiyo leo jijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...