Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

KLABU ya Soka ya Yanga imewarudisha waliowahi kuwa Makocha wake Wakuu kwa vipindi tofauti, Mwinyi Zahera na Cedric Kaze ambao wamerejea Kikosini hapo katika majukumu tofauti msimu huu wa mashindano.


Mwinyi Zahera amerejea Yanga SC kama Mkurugenzi wa Maendeleo Soka la Vijana, awali Zahera alikuwa Kocha Mkuu wa Klabu hiyo, Cedric Kaze pia amewahi kuwa Kocha Mkuu Kikosini hapo, kwa sasa amerejea kama Kocha Msaidizi chini ya Kocha Mkuu Nasreddine Nabi.
 

Kupitia kurasa zao za Mitandao ya Kijamii, Yanga SC imetoa taarifa ya kuwatambulisha Makocha hao Kitaaluma kuisaidia Klabu hiyo kuanzia timu za vijana hadi timu kubwa.


Yanga SC itashuka dimbani kesho Jumamosi ya Septemba 25, 2021 katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba SC. Mchezo huo mahsusi kufungua pazia la Ligi Kuu Soka Tanzania Bara msimu mpya wa 2021-2022.

Kocha Mkuu wa Yanga SC, Nasreddine Nabi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Kocha Msaidizi wa Klabu hiyo, Cedric Kaze (kulia) na Mkurugenzi wa Maendeleo Soka la Vijana, Mwinyi Zahera (kushoto).
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...