Italia imesema itaweka msukumo wa kuzisaidia nchi za Bara la Afrika na zile zinazoendelea kuweza kutengeneza chanjo ya magonjwa mbalimbali ikiwemo ya UVIKO -19 ili kuweka usawa wa upatikanaji wa chanjo pale kunapotokea milipuko ya maradhi.

 

Rais wa Italia Mhe. Sergio Mattarella ameyasema hayo katika Mkutano wa tatu wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Afrika na Italia ambao uliopewa jina la Encouters with Africa 2021 ambapo ameeleza kusikitishwa kwake na idadi ndogo ya watu waliopata chanjo katika Nchi za Kiafrika ambapo mpaka sasa ni asilimi 2 hadi 3 ya Waafrika wote waliopata chanjo ya UVIKO -19.

 

Akizungumza mara baada ya mkutano huo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula amesema mbali na msisitizo uliowekwa katika kuiwezesha Afrika kutengeneza chanjo pia Italia imesema kuna umuhimu wa Bara la Afrika kupitia Umoja wa Afrika kushiriki kikamilifu kama mwanachama wa kundi la G20 na hivyo kuunda kundi jipya la G21 tofauti na sasa ambapo Afrika inashiriki katika mkutano wa G20 kama mwalikwa

 

Balozi Mulamula amesema pia amelitumia jukwaa hilo la Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za Afrika na Italia kuelezea vipaumbele vya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuelezea azma ya Tanzania kuthamini ushirikiano na Mataifa mengine pamoja na Jumuiya za Kimataifa ikiwa ni pamoja na ushirikishwaji na uwazi katika kupambana na ugonjwa wa UVIKO 19,kuoambana na mabadiliko hasi ya tabianchi pamoja na usawa wa kijinsia.

 

Akizungumza kwa niaba ya Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika,Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika  ameyataka Mataifa yaliyoendelea kuweka msukumo kwa makampuni yanayotengeneza chanjo ya UVIKO -19 kutoa kibali kwa Mataifa ya Afrika kuweza kutumia teknolojia yao katika kutengeneza chanjo ya ugonjwa huo ili kuliwezesha Bara la Afrika kuweza kutoa chanjo kwa asilimia kubwa ya Wananchi wake tifauti na ilivyo sasa ambapo hakuna usawa katika upatikanaji wa chanjo hiyo.

 

Mkutano huo wa siku mbili umewakutanisha Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za Afrika zaidi ya 50 ambapo Italia imeweka msisitizo wa kushirikiana na Nchi za Afrika katika masuala ya biasahara,uwekezaji na ubadilishanaji wa teknolojia badala ya kutoa misaada kama ilivyozoeleka.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...