Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
Msanii Bongo Fleva nchini, Ali Saleh Kiba maarufu King Kiba rasmi amedondosha ‘Album’ yake mpya iliyopewa jina la ONLY ONE KING ambayo imezinduliwa jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Wasanii kedekede nchini wakiwemo Wasanii wa kigeni, Patoranking wa Nigeria na Maud Elka kutoka DR Congo.
Katika uzinduzi wa Album hiyo, King Kiba amejumuisha jumla ya Nyimbo 16 baadhi zilizoshirikisha Wasanii mbalimbali wakiwemo Rappers. King Kiba ameweka wazi utunzi wa nyimbo hizo kushirikiana na timu yake ya Kings Music Record Lebo, ametaja changomoto ya kuchelewa kutoka kwa Album hiyo, ni upatikanaji wa Wasanii walioshiriki kwenye baadhi nyimbo zake.
Album hiyo ni ya Tatu kwa Msanii huyo ikiwa ni miaka 18 tangu aingie rasmi kwenye Muziki wa Bongo Fleva. Pia amesema uzinduzi huo umeenda sambamba na kuwakutanisha yeye na watu wengine waliokuwa karibu naye, pia baadhi ya watu aliokuwa nao tangu kuanza safari yake ya Muziki.
“Ahsanteni sana Vyombo vya Habari nchini, mmekuwa na mchango mkubwa sana katika Muziki wa Tanzania, tunawashukuru sana Waandishi wa Habari kupitia Vyombo vyenu vyote vya Habari, Vyombo vya Habari vina nguvu sana”, amesema King Kiba katika uzinduzi huo.
Nyimbo 16 zilizojumuishwa kwenye Album hiyo ni Oya Oya, Amour, Tamba, Jelous, Sitaki Tena, Salute, Washa, Infidèle, Bwana Mdogo, Habibty, Gimme Dat, Niteke, Let Me, Utu, Ndombolo na Happy.
Hiyo ni Album ya tatu kwa King Kiba tangu kuanza Muziki, Album nyingine ni ALI 4 REAL na CINDERELLA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...