Mwanachama wa ATD na Mwenyekiti wa kamati ya maadhimisho hayo Venance Magombera (Kushoto,) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maadhimisho ya siku ya kupambana na umaskini duniani yatakayofanyika Oktoba 24 katika kituo cha utamaduni cha Alliance Francaise jijini Dar es Salaam.



* Vikundi vya ujasiriamali vyaushukuru Ubalozi wa Ufaransa, Alliance Francaise na Serikali kwa ufadhili wa miradi ya maendeleo


KITUO Cha Utamaduni cha Ufaransa (Alliance Francaise,) kwa kushirikiana na ubalozi wa Ufaransa nchini na shirika lisilo la kiserikali la kimataifa la ATD (All Together in Diginity- Fourth World,) pamoja asasi mbalimbali zinazohusu wanawake katika mapambano dhidi ya umaskini za Iloganzara Women Agaist Poverty (IWAPOA,) na chama cha ujasiriamali cha wanawake wa Tandale, Boko na Temeke (TABOTE) wanatarajia kuadhimisha siku ya mapambano dhidi ya umaskini jumapili ya Oktoba 24 katika kituo hicho huku huku wanawake wakipewa nafasi zaidi ya kushiriki kupitia asasi mbalimbali za ujasiriamali kwa wanawake.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam mwanachama wa ATD na mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya maadhimisho hayo Venance Magombera amesema, maadhimisho hayo ni kwa ajili ya watu waishio katika hali ya umaskini na ufukara uliopitiliza ambao hawana msemaji kwa falsafa ya ATD ya 'Sote kwa pamoja katika utu, Dunia ya nne kwa nchi zote zinazoendelea na zilizoendelea ambazo bado kuna wimbi kubwa la umaskini na ufukara uliopitiliza.

Amesema, maadhimisho hayo yaliidhinishwa na umoja wa mataifa mwaka 1992 na huadhimishwa kila Oktoba 17 kwa wanachama wa ATD kushirikiana na makundi mbalimbali kwa watu waishio kwenye wimbi la umaskini na ufukara uliopitiliza kupaza sauti juu ya hali zao za maisha na majukumu wanayoyaafanya kila siku katika kujikwamua na wimbi hilo.

Magombera amesema, ATD shirika lisilo la kiserikali la kimataifa lina maono ya kuiweka dunia bila umaskini na kuheshimiwa kwa kila mtu na kupata haki zao za msingi pamoja na kutambulika kwa shughuli za kiuchumi wanazozifanya katika kupambana na wimbi la umaskini.

'' ATD inafanya kazi katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam; Tandale, Mwananyamala na soko la samaki Feri na machimbo ya kokoto Boko ambapo wanawake katika maeneo hayo wamepewa elimu na mafunzo maalumu na wameweza kujikwamua kwa kufanya shughuli za kiuchumi ikiwemo utengenezaji wa sabuni, usukaji wa vikapu pamoja na shughuli nyingi zinazowaingizia kipato.'' Amesema.

Aidha amesema kuwa ATD kwa kushirikiana na ubalozi wa Ufaransa na kituo cha utamaduni cha Alliance Francaise wamekuwa wakitoa ushirikiano hasa kwa kubaini maeneo yaliyoathirika zaidi na wimbi la umaskini na kufadhili mitaji katika vikundi vya wanawake katika maeneo mbalimbali ikiwemo katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Mbeya na Njombe na wana miradi mbalimbali inayohusisha wanawake ikiwemo ya elimu na mafunzo ambayo imezaa matunda na Serikali kuonesha ushiriki.

Vilevile Magombera amwataka wananchi kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita, umoja wa kimataifa na asasi za kiraia katika kupiga vita adui umaskini.

kwa upande wake Mwenyekiti asasi ya IWAPOA ambayo ni zao la ATD Paskazia Senzari amesema asasi hiyo ilianza 2008 baada ya kugundua changamoto zinazowakumba wanawake, wajane na jamii kwa ujumla hasa kwa watu waishio na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na kituo cha utamaduni cha Alliance Francaise na Ubalozi wa Ufaransa nchini wamekuwa wafadhili wa kubwa katika kuwakwamua wanawake kupitia shughuli mbalimbali ikiwemo utekenezaji wa sabuni za kuogea, kufulia pamoja na bidhaa za batiki, vikapu na elimu ya utunzaji wa fedha (kuweka akiba.)

Paskazia amesema, ubalozi wa Ufaransa kupitia kituo hicho walitoa ufadhili kwa wanawake 150 waliopata mafunzo mbalimbali ya ujasiriamali na wameweza kujiajiri hatimaye Serikali kuwaamini kuwapa mkopo kwa asilimia nne kupitia vikundi vyao.

Amesema wakazi wa Dar es Salaam wajitokeze kwa wingi katika maadhimisho hayo kujionea mwamko wa wanawake na shuhuda za wanawake waliofanikiwa na ameushukuru Ubalozi wa Ufaransa kupitia kituo hicho ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kufadhili miradi hiyo.


Katibu wa asas ya IWAPOA Anna Mango akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maadhimisho hayo na kueleza kuwa walitumia muda mrefu kutoa elimu kwa wanawake ambao sasa wanafanya shughuli zao za kijamii na kuweka akiba za ziada kwa matumizi ya baadaye, leo jijini Dar es Salaam.




Mwenyekiti wa asasi ya IWAPOA Paskazia Senzari (kulia,) akizungumza na waandishi wa habari katika kuelekea maadhimisho ya siku ya kupambana dhidi ya umaskini duniani na kueleza kuwa Ubalozi wa Ufaransa kupitia kituo cha utamaduni cha Allience Francaise kimefadhili wanawake 150 waliopata elimu ya ujasiriamali, leo jijini Dar es Salaam.






Matukio mbalimbali katika hafla maalumu kuelekea maadhimisho ya siku ya kupambana na umaskini duniani yatakayofanyika Oktoba 24 mwaka huu jijini Dar es Salaam.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...