Mwakilishi wa wa Ubalozi wa Ubelgiji nchini, Jasmien De Winne akikata utepe kuashiria kuzinduliwa kwa maabara ya kisasa ya kufundishia teknolojia ya uendeshaji wa mitambo ya viwandani ya Chuo Kikuu Ardhi (ARU), kwenye hafla iliyofanyika chuoni hapo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mkufunzi kutoka Ubelgiji, Dirk Van Merode, akielezea namna maabara hiyo ya kisasa inavyofanya kazi wakati wa uzinduzi wa maabara hiyo uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam katika Chuo Kikuu Ardhi (ARU).
ageni mbalimbali wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kuzinduliwa kwa kuzinduliwa kwa kimepata maabara ya kisasa ya kufundishia teknolojia ya uendeshaji wa mitambo ya viwandani ya Chuo Kikuu Ardhi (ARU), kwenye hafla iliyofanyika chuoni hapo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu

CHUO Kikuu Ardhi (ARU), kimepata maabara ya kisasa ya kufundishia teknolojia ya uendeshaji wa mitambo ya viwandani.

Maabara hiyo imezinduliwa mwishoni mwa wiki chuoni hapo jijini Dar es Salaam na Mwakilishi wa wa Ubalozi wa Ubelgiji nchini, Jasmien De Winne na Naibu Makamu Mkuu wa chuo hicho Taaluma, Profesa Gabriel Kassenga.

Maabara hiyo ambayo imejengwa kwa ufadhili wa serikali ya Ubelgiji imegharimu Euro 47,000 zilizojumuisha kutengeneza maabara na mafunzo kwa wakufunzi.

 Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Profesa Kassenga amesema itasaidia kufundisha wanafunzi masuala ya umeme viwandani hasa wakati huu wa uchumi wa viwanda.

Amesema maabara hiyo pia itasaidia wanafunzi wapate ujuzi wa kufanyakazi viwandani na kupata tija na kwamba haitatumika na ARU peke yake bali kwa vyuo vingine vinavyofundisha masuala ya uendeshaji wa viwanda ili wapate uwezo wa kuingia kwenye soko la ajira.

Kwa upande wake, Mhadhiri Msaidizi wa ARU, Mhandisi Godfrey Luwemba amesema maabara hiyo ya teknolojia ya uendeshaji wa viwanda chuo kilipata mradi kutoka Kamisheni ya Ulaya kuhusu kuleta vifaa kufundisha uendeshaji wa viwanda.

Amesema baada ya kupata mradi huo waliandaa mitaala kwaajili ya kukidhi mahitaji ya Afrika Mashariki kwani kuna vyuo ambavyo ARU inafanyakazi navyo vya Uganda na Ethiopia na baadhi ya nchi za Ulaya kama Ubelgiji.

“ Kama nchi kwa maendeleo yaliyopo sasa tuliangalia pengo la ujuzi kuhusu uendeshaji wa viwanda kwa kutumia kompyuta hivyo lengo ni kuziba hilo pengo la wataalamu wa uendeshaji viwanda kwa kutumia kompyuta,” amesema

Amesema kupitia maabara hiyo wanafunzi watafaidika kwa kupata ujuzi ambao utawasaidia wao binafsi, nchi na watu wenye viwanda kupata wataalamu wa kuendesha mitambo ya viwanda vyao kwa kutumia kompyuta.

“Kwa utaalamu huo utakapopatikana tunaamini ARU itachangia kwa kiasi kikubwa kuongeza wataalamu wenye ujuzi wa kuendesha viwanda kwa kutumia kompyuta na kukuza viwanda na taifa litanufaika sana na idadi kubwa ya wataalamu watakaozalishwa kutoka kwenye hii maabara,” alisema.

ARU ni moja ya vyuo vilivyofaidika kati ya vyuo sita kutoka nchi za Tanzania, Uganda na Ethiopia chini ya mradi wa Applied Curriculum in Technology for East Afrika (ACTEA), ambapo baadhi ya washiriki kwenye mradi huo wamepata mafunzo ya siku tano kuwapa uwezo wa kutumia vifaa hivyo katika kufundishia.

Washiriki wa mafunzo hayo ni wahadhiri kutoka vyuo vingine ambao nao ni wanufaika ikiwemo Mzumbe, Chuo Kikuu Muni, Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbarara Uganda na Chuo Kikuu Jimma cha Ethiopia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...