Benki ya
Exim imezindua kampeniya ‘Weka Mkwanja Tukutoe!’inayolenga kuhamasisha
watanzania kujiwekea amana huku wakipata fursa za kunyakua zawadi
mbalimbali ikiwemo fedha taslimu pamoja na gari aina Toyota Vanguard.
Kampeni
hiyoya miezi mitatu inayofahamika kama ‘Weka mkwanjatukutoe!’
imezinduliwa leo jijini Dar es Salaam na imepangwa kuwafikia watanzania
wote wakiwemo wateja wa benki hiyo pamoja na wale watarajiwa.
Akizungumza
wakati hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo jijini Dar es Salaam leo, Mkuu
wa Huduma ya wateja Rejareja na wajasiriamali wa Benki ya Exim, Bwana
Andrew Lyimo alisema kampeni hiyo inalenga kuleta mabadiliko kwenye
mtazamo wa uhifadhi wa amana miongoni mwa watanzania kutoka kuhifadhi
pesa majumbani na badala yake wazihifadhi kupitia benki hiyo kwa usalama
wa fedha zao sambamba na faida nyingine nyingi ikiwemo riba.
“Lengo
si tu kuhamasisha watanzania kujenga utamaduni wa kujiwekea amana,
tunachohitaji ni kuona kwamba Watanzania wengi wanajiwekea amana zao
sehemu salama ili kujiendeleza kukua kiuchumi ndio maana tumejipanga
kuwahamasisha watumie akaunti zetu mbalimbali ikiwemo akaunti ya
mshahara inayotumika kwa matumizi mbalimbali ya kila siku,’’
“Nyingine
ni akaunti ya mzalendo inaendeshwa bila makato ya kila mwezi, akaunti
ya haba na haba, akaunti ya faida hizi zinakuruhusu kuweka akiba na
kupata riba, tuna akaunti ya Nyota ambayo ni akaunti maalum kwa ajili ya
kuwawekea Watoto akiba ya badae na mwisho kabisa tuna akaunti ya
wajasiriamaliinayowahudumia wafanyabiashara na mahitaji yao tofauti
tofauti ya kibiashara ’’ alisema Bw. Lyimo.
Akitaja zawadi
zikazotolewa kupitia akaunti hiyo, Bw. Lyimo alisema ni pamoja na zawadi
za fedha taslimu kiasi cha Tsh. milioni 1, kwa mwezi na kila mwezi
kutakua na washindi sita, sambamba na kuingia kwenye droo
itakayowawezesha kushinda zawadi kubwa ya gari aina ya Toyota Vanguard.
“Hivyo basi wateja wetu wa sasa na wale wapya watakuwa kwenye nafasi ya
kujishindia zawadi hizi kila wakapojiwekea akiba ya kuanzi Tsh. 500,000
na kuendelea. Kadili wanavyojiwekea amana kubwa zaidi ndivyo
wanavyojiweka kwenye nafasi ya kushinda zawadi kubwa zaidi,’’ alisema.
Mkuu wa Huduma ya wateja Rejareja na wajasiriamali wa Benki ya Exim, Bwana Andrew Lyimo (katikati) sambamba na wafanyakazi wengine wa benki hiyo wakionesha ufunguo wa gari aina ya Toyota Vanguard (inayoonekana nyuma) itakayotolewa kwa mshindi wa kampeni mpya ya benki hiyo inayofahamika ‘Weka Mkwanja Tukutoe!’inayolenga kuhamasisha watanzania kujiwekea amana wakati wa hafla fupi ya unzinduzi wa kampeni hiyo jijini Dar es Salaam jana.
wafanyakazi wa benki ya Exim wakionesha gari aina ya Toyota Vanguard itakayotolewa kwa mshindi wa kampeni mpya ya benki hiyo inayofahamika ‘Weka Mkwanja Tukutoe!’inayolenga kuhamasisha watanzania kujiwekea amana wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa kampeni hiyo jijini Dar es Salaam jana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...