Na Khadija Kalili, Kibaha
MKUU wa Wilaya ya Kibaha Sara Msafiri ametoa wito kwa wanawake wa Mkoa wa Pwani kuzithamini kazi zao mdogomdogo ambazo ndizo zinajenga uchumi wa familia na nchi kwa ujumla kujenga utamaduni wa kunyanyuana.
"Nawasihi wale ambao mnafanya biashara ndogo ndogo kunyanyuana kama jinsi ambavyo serikali yetu ya awamu ya sita inavyoweka kipaumbele kwa wanawake huku tukiwa tumepata bahati ya kuwa Rais mwanamke Samia Suluhu Hassan kwakuwa amekuwa anazungumzia wanawake kila mahali anapokuwa "alisema DC Msafiri.
DC alisema hayo jana jioni alipokuwa mgeni rasmi kwenye kongamano la wanawake lilifahamika kwa jina la 'Fursa Gala' lililowakutanisha wanawake wa kada mbalimbali kutoka katika Wilaya za Mkuranga, Kibaha, Chalinze ,Mlandizi na Bagamoyo lililofanyika kwenye ukumbi wa Destiny uliopo Kwa Mathias Kibaha Mkoani Pwani.
"Kama Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan anavyohimiza utalii wa ndani na sisi tutandaa wiki ya mjasiriamali Kibaha Ili tuweze kupeana fursa na ninaamini tutaweza " alisema DC Sara.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama Mahala pa Kazi (OSHA) Khadija Mwenda amesema kuwa amevutiwa na mwitikio wa wanawake wa Mkoa wa Pwani jinsi walivyojitokeza kwenye Kongamano hilo huku akiwaahidi kurudi na kuwatembelea na kwakagua katika maeneo yao ya kazi huku akipanga kuwapa elimu ya kutosha juu ya usalama wao mahali pa kazi.
"Nawasisitiza kina mama kuwa makini katika maeneo yenu ya kazi kwani hakuna shughuli yote ya kiuchumi ambayo haina athari ya kiusalama wa afya mfano ni kwa watengenezaji wa batiki na sabuni na bidhaa zingine wengi hawana elimu ya usalama wa afya zao mahala pa kazi hivyo sisi kama OSHA tutatengeneza mpango wa kuwatembelea wajasiriamali wote tutawashauri na kwakagua" alisema Khadija.
Naye Mwanasaikolojia mbobevu aliyekuwa Mwezeshaji Dkt. Eli Waminian amewataka wanawake kuwekeza fikra zao katika kujiamini kwa sababu mwanamke ndiyo ngome kuu hapa duniani na dunia haiwezi kukamilika bila ya kuwepo mwanamke hivyo wajiamini katika kilajambo wanalolifanya watafanikiwa huku aliwataka wawe na fikra chanya na kutoamini katika kushindwa.
"Mwanamke ni sawa na ardhi na hii ni sayari yake hivyo wanawake waache tabia za kuwa na malalamiko, pia amewataka wanawake kuwaunganisha watoto wao na jamii kama jinsi ilivyokuwa zamani leeni watoto kwa kuwaunganisha na jamii Ili hata kama ukifa leo mtoto wako aweze kuishi maisha bila uwepo wako kwani hutoweza kyishi nae milele" alisema Dkt. Eli ambaye amekuwa akiivutia jamii kutokana na mafundisho yake anayoyatoa kwa jamii katika makongamano mbalimbali.
Kongamano hilo limeandaliwa na Kampuni mbili ambazo ni HEROCHIC Suzana Mdonya kwa kushirikiana na Vitenge na Tamrah Kibaha inayoongozwa na Nyamizi Yasin.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...