Na Mwandishi wetu,
Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) imewahamasisha wanafunzi wa kike zaidi ya 860 wa shule 17 za Sekondari katika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma kusoma masomo ya sayansi kuchochea dhana ya Tanzania ya Viwanda.
Aidha, uhamasishaji huo utasaidia kuongeza udahili wa wanafunzi wa kike katika Taasisi hiyo DIT inazunguka kufanya uhamasishaji kwa wanafunzi wa Sekondari za mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma, Njombe, Mbeya na Iringa kusoma masomo ya Sayansi.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma, Dk. Frederick Sagamiko ameishukuru timu ya DIT kwa ziara hiyo, ametoa wito kwa wasichana kusoma masomo ya Sayansi kwa bidii nchi ipate wanasayansi wa kutosha.
Dk Sagamiko alitumia fursa hiyo kuiomba DIT kushirikiana na Manispaa hiyo kuhamasisha wasichana wapende masomo ya Sayansi.
"Mkoa wa Ruvuma una Halmashauri 8 wasichana ni wengi, walioko mijini wanapata nafasi nyingi za kusikia na kupata taarifa mbalimbali kuliko wa vijijini, tuangalie kuwafikia wasichana wengi zaidi walioko vijijini, ofisi yangu iko tayari kushirikiana na DIT kutoa elimu hii" amesema.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Dr Fredrick Damas Sagamiko akiongea na wanafunzi
Dr. Triphonia Ngairo Afisa Udahili wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT). Akiwatoa maelezo juu ya kozi zinazotolea na DIT na vigezo vya Udahili.
Afisa Elimu Manispaa ya Songea alikuwa anamkaribisha mkurugenzi aongee na wanafunzi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...