Makamu wa Rais, Dkt. Phillip Mpango (katikati) akikata utepe ikiwa ni ishara ya kukabidhi magari 18 na pikipiki 20 kwa Shirika la Posta Tanzania (TPC) kwa ajili ya kuboresha huduma za shirika hilo. Tukio hilo lilifanyika wakati wa kuhitimisha maadhimisho ya Wiki ya Posta Duniani lililofanyika kitaifa katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete (JKCC) jijini Dodoma. Kushoto kwake ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari (WHMTH) Dkt. Ashatu Kijaji na kulia kwake ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dkt. Zainab Chaula.
Dkt Mpango akishuka kutoka kwenye gari hilo.
Makamu wa Rais, Dkt Mpango akimkabiudhi tuzo Mwanafunzi wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari Msalato, Renalda Reginald kwa kuwa mshindi wa kuandika insha kuhusu matumizi ya huduma mpya ya kidigitali.
Dkt. Mpango akimkabidhi tuzo mwanafunzi Faraja Robert (asiyeona) wa shule ya Buhangija ya Shinyanga baada ya kuwa mshindi wa tuzo maalumu kwa wanafunzi walioandika insha nzuri.
Dkt Mpango akimkabidhi tuzo ya cheti mwakilishi wa Benki ya CRDB wadhamini wakuu wa maadhimisho hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamis Munkunda (kushoto) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Gift Msuya.
Kaimu Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Macrice Mbodo akielezea mikakati mbalimbali waliyofanya kuboresha huduma za shirika hilo ikiwemo uanzishwaji wa Duka la Posta Mtandaoni ambapo limeungana na maduka 670 duniani ambapo wateja wanunua na kuuza bidhaa zao mtandaoni.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU), Sifundo Moyo akitoa salamu za umoja huo wakati wa maadhimisho hayo.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt Kijaji akizungumza maneno ya utangulizi kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais, Dkt. Mpango kuhutubia na kuhitimisha maadhimisho hayo.
Mbunge wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu akijadiliana jambo na Waziri Dkt Kijaji na Katibu Mkuu, Dkt Chaula.
Baadhi ya pikipiki zilizokabidhiwa kwa TPC kwa ajili ya kuboresha huduma ya shirika hilo.
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...