Na Khadija Kalili , Rufiji
Naibu Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson amesema kuwa anatambua na kuthamini mchango wa aliyekuwa Mwenyekiti wa kwanza wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Hayati Bibi Titi Mohammed ambaye alikua mwanachama namba 16 pia mpigania Uhuru alikua mwanamke pekee atakayebaki katika historia ya kupigania Uhuru wa nchi ya Tanzania hivyo tukiwa tunaelekea kusherehekea miaka 60 ya Uhuru kumuenzi ni wajibu wa Kila mtanzania.
"Katika kusherehekea maisha yake Hayati Bibi Titi tunatambua mchango wake mkubwa ndani ya taifa hili na juhudi zake ndizo zilizo tufikisha sisi viongozi wanawake hapa tulipo" alisema Naibu Spika Dkt. Tulia
Dkt. Tulia alisema hayo alipozungumza katika mahojiano na Michuzi Blog kuwa hivi sasa nchi imekuwa na viongozi wengi wa kike kutokana na hamasa za Bibi Titi ambazo alizitoa kwa kina mama wa kitanzania pamoja na kina baba pia ambao alikuwa nao bega kwa bega katika harakati za kudai Uhuru.
"Bibi Titi ni bibi yetu ni yeye alisaidia katika juhudi za kupigania Uhuru wa nchi yetu na kuhakikisha heshima yake inakuwepo hivyo na sisi hatuna budi kumuenzi na kuthamini mchango wake"alisema Dkt. Tulia .
Tulipofikia sasa hivi mwanamke anaweza kujitambua kwani mwanamke ana uwezo wa kuweza kufanya kazi kama mwanaume na hili alilianzisha yeye enzi hizo kiwa kijana aliweza kufanya kazi began kwa bega na wanaume hali ambayo ilimjengea Imani kubwa kwaaliyekuwa Rais wa Kwanza wa nchi hii Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Dkt. Tulia alisema kuwa kwa mustakabali huo wa sifa za ushupavu wa Hayati Bbi Titi viongozi wote wanaowajibu wa kuendeleza juhudi zilizoanzishwa na kufanyiwa na bibi Titi huku alisisitiza kuwa nyayo hizo zinafuatwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.
Wakati huohuo alisema kuwa anaiomba serikali kuweka mkakati wa kuzalisha kina Bibi Titi wengine huku alifafanua namna ya kuwazalisha ni pale mwanamke anapopata fursa za. kazi wazitumie vizuri na kuweka rekodi katika ufanisi wa kazi.
Akizungumzia kuhusu Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT),kuamua kilele chake kufanyika Ikwiriri Wilayani Rufiji Mkoa wa Pwani alisema kuwa siku ya leo Oktoba 23 ni muhimu na siku kubwa katika bara la Afrika , ikumbukwe kuwa bibi Titi ni muasisi na katika enzi hizo haikuwa jambo rahisi mwanamke kujitokeza hadharani na kupambania kile alichokiamini kuwa ni haki yake lakini yeye alipambana hadharani bila woga.
Aidha Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Pwani Mama Salma Kikwete alisema.kuwa maadhimisho ya wiki ya UWT Taifa kufanyika Rufiji ni jambo ambalo limempa faraja kubwa huku alisisitiza kuwapa vipaumbele watoto wa kike bila.kuwasahau watoto wa kiume kwani na wao wana uhitaji hivyo ni wajibu wote kupewa malezi mazuri ikiwemo kuwapa Elimu ya kutosha Ili wote kwa pamoja waweze kutimiza ama kufikia njozi zao katika maisha.
Alisema wakati alipokuwa Mwalimu aligundua kuwa wanafunzi wa kike wana usomaji na uelewa uliojaa changamoto nyingi ndipo alipopata fursa akaanzisha Taasisi ya WAMA huku lengo kubwa likiwa ni kumkomboa mtoto wa kike kieleimu.
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan aliyekuwa mgeni rasmi katika kilele cha wiki ya UWT alimmwagia sifa Bibi Titi kwa kusema kuwa licha ya Leo kwamba anasifiwa lakini wakati akiwa anapigania uhuru na maslahi ya nchi kwa ujumla wapo watu ambao walimbeza na kumkejeli lakni yeye alikuwa mwanamke shupavu Kamwe yale maneno hayakuweza kumrudisha nyuma na kufifiza harakati zake.
Kwa mantiki hiyo basi amewataka wataalamu wa Uandishi wa historia waweze kuketi na kuandika masuala yenye historia za nchi Ili kuweza kusaidia Kizazi kijacho kutambua historia ya nchi Yao ikiwemo wanaharakati mbalimbali ambao waliweza kuchangia kuleta uhuru wa nchi akiwemo Bibi Titi Mohammed.
Rais Samia alitoa wito kwa UWT kuongeza miradi mingi Ili waweze kujitegemea, pia alisema amezisikiliza changamoto walizonazo hivyo atakaa na viongozi watajadili kwa pamoja namna ya kuweza kuzitatua huku alisisitiza wanawake kushikamana na kuacha tabia ya kuchochea chuki miongoni mwao katika maeneo mbali mbali ikiwemo maeneo ya kazi kuacha makundi huku akiwataka kushikana na kuwa walezi bora wa familia kwa ujumla.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...