* Wapangiwa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 11.6
* Idadi ya wanufaika mwaka wa kwanza yafikia 65,359
* Orodha ya tano kutangazwa wiki ijayo


BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB,) imetangaza orodha ya nne yenye wanafunzi wanufaika wapya 5,003 wa mwaka wa kwanza waliopangiwa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 11.6 huku orodha ya tano ikitegemewa kutangazwa wiki ijayo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati akitangaza orodha ya nne ya wanufaika wa mkopo Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Abdul-Razaq Badru amesema, hadi sasa jumla ya wanufaika wa mwaka wa kwanza imefikia 65,359 ambao wamepangiwa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 168.9.

''Orodha hii ya nne ina wanufaika 5,003 ambao muda wowote kuanzia sasa wanaweza kuingia katika akaunti zao za SIPA walizoombea mkopo na kupata taarifa zaidi.'' Amesema Badru.

Badru amesema, wanufaika hao 65,359 wanufaika 1,133 ni yatima waliofiwa na wazazi wawili, 9,450 wamefiwa na mzazi mmoja , wanafunzi 198 ni wenye wanafunzi wenye ulemavu, 2,919 walifadhiliwa na taasisi mbalimbali katika masomo yao ya Sekondari na wanafunzi 51,559 wanatoka katika kaya masikini.

''Kwa takwimu hizi, mtaona kuwa ile dhamira ya Serikali ya kuwawezesha vijana kutoka kaya masikini inathibitika'' Amesema Badru na kuongeza kuwa asilimia 41 ya wanufaika 65,359 ni wanawake na asilimia 59 ni wanaume. Na kueleza kuwa kiwango cha chini ya mkpo ni shilingi milioni mbili na laki moja huku kiwango cha juu cha mkpo kikiwa ni shilingi milioni sita na laki nne.

Kuhusiana na mikopo kwa wanafunzi wanaoendelea na masomo Badru amesema, HESLB inakamilisha maombi ya wanafunzi 74,440 ambao ni wanufaika wanaoendelea na masomo baada ya kupokea matokeo yao ya mitihani inayoonesha wamefaulu na kuendelea na masomo yao.

''Tuna wanufaika zaidi ya 98,000 wanaoendelea na masomona hadi leo (Ijumaa ya Oktoba 29,2021,) Tumepokea matokeo ya mitihani ya wanafunzi 74,440 waliofaulu na tutaanza kutuma fedha kesho.'' Amesema Badru na kuvikumbusha vyuo kuwasilisha matokeo kwa wanufaika waliobaki.

Kuhusiana na rufaa kwa wanafunzi Badru amesema, dirisha la rufaa litafunguliwa Novemba 6, 2021 ili kuwapa fursa wanafunzi ambao hawajaridhika na viwango vya mkopo walivyopangiwa kwa kuwasilisha maombi ya kuongezewa na kwa wanafunzi wanaoendelea na masomo walioomba mkopo orodha ipo tayari kukamilika na itatolewa siku chache zijazo baada ya kujiridhisha uhitaji wao uthibitisho wa ufaulu wao mitihani yao kupitia matokeo yaliyowasilishwa kwao.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...