Na.Vero Ignatus,Arusha.
Mkutano wa tano Mwaka wa TEHAMA unaendelea Jijini Arusha ,ukiwa na lengo la kuwaunganisha wadau wote wa tehama,kutoka sekta za Umma na Binafsi ili kujadiliana Maendeleo ya Tehama Nchini
Neema Lugangira Mbunge wa viti Maalum (CCM) ambaye anawakilisha Asasi za Kiraia NGO kutoka Tanzania Bara, amesema kwamba suala la kunufaika katika tehama ni pamoja na Ushirikishwaji wa makundi yote wakiwemo wanawake ,kwani kumekuwa na ukuaji mkubwa wa ukatili wa Kijinsia kwenye mitandao ya kijamii
Tunapoongelea ukuaji wa kidigitali lazima tuangazie Usalama kwenye mitandao ya kijamii kwa makundi yote ikiwemo kundi la wanawake kwenye siasa.Alisema Rugangira(Mb)
Lugangira amesema kuwa Jambo hilo limekuwa kisababishi ambacho vinapelekea wanawake kuogopa kuingia kwenye siasa,maana wanajua wakiingia hawatakinzana kwa hoja bali watu kwenye mitandao watajibi,ana nao kutokana na uanawake wa mtu husika
Mimi nikiwa Kama mwanamke kwenye siasa (mb)nimejaribu kuwaeleza wadau wa ICT iko haja ya kuangalia Ukatili wa Kijinsia unaowekwa kwenye wanawake walioko kwenye siasa,kwani ni kati ya ,hivyo inapelekea ushiriki wawanawake kwenye siasa ,unakuwa mdogo,pia inapelekea wale wanaotamani kuingia kwenye siasa wanahofu ya kuingia kwenye siasa.Alisema Rugangira
Sambamba na hayo ametoa pendekezo kwa ICT Kuona nchi inakuwa na Sera za uchumi kidigitali ,Sera mkakati na mfumo ambao utapelekea ukuaji wa sekta ya Tehema
Tukikinfanisha na wenzetu wa Kenya wanazonsera hizi zote,na wao kwenye taarifa zao rasmi unasema kwamba hii sekta ya digitali inachangia kwa 8%kwenye Pato ghafi,lakini pia inatengeneza ajira zaidi ya 250,000,vilevile ndio sekta inayokua kwa Kasi" Alisema Neema(Mb)
Akizungumza na waandishi wa habari MKURUGENZI wa TEHAMA Mulembwa Munaku ,kutoka Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya habari ambae pia ni mwenyekiti wa Kongamano hilo,amesema kuwa kwa Sasa hivi yapo mabadiliko makubwa ya tehema nchini na mtu anaweza kutumia simu yake ya mkononi na akafanya biashara ya mtandaoni
Munaku ametoa wito kwa Wazazi wote na Jamii kwa ujumla ,waweze kuhakikisha kwamba, vijana wanatumia tehama kwa mtumizi sahihi ili iwasaidie katika makuzi yao,kwa kutafuta fursa mbalimbali za kipato na kiuchumi
Akijibu swali aliloulijwa juu ya ukuaji wa Tehama na athari kwa vijana :Changamoto kubwa haswa ipo kwa vijana 75% hivyo Kama wanahitaji kujenga Taifa sahihi lenye mahitaji ya tehama ,lazima tujikite Kama Serikali tuwekeze tuangalie ni namna gani tutawasaidia vijana
Munaku alisema kutokana na changamoto hizo wamejipanga na kuwaunganisha wadau na kuanza kupeleka na kuongeza Elimu kwa vijana ,kwa matumizi ya tehama, pia wananchi wanapaswa kufahamu kuwa siyo jukumu la Serikali pekee, bali kila mdau anawajibika kuanzi ngazi ya shuleni,familia kuhakikisha kijana aliyenae nyumbani aweze kukutumia katika njia iliyo sahihi.
Alisisitiza kuwa Matarajio ya wananchi ni kupata elimu, ambayo kama Taifa lilivyopiga hatua katika masuala ya Tehama, mtandao,pia watarajie kuangalia namna watakavyopata wawekezaji katika tehama,na mazimio ambayo watayapata kwenye kikao hicho ,watayafanyia kazi ili waweze kupiga hatua kwa kuwasaidia wananchi na kuongeza ajira
Aidha mkutano huo wa siku tatu unaendeleaje Jijini Arusha katika Kituo Cha Kimataifa Cha AICC,umehudhuriwa na wadau zaidi ya wadau 600 ,wengi wao wamejiunga kufuatilia kwa kupitia njia ya mtandao,ambapo utafunguliwa na kufungwa hapo siku ya ijumaa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kasimu Majaliwa.
Mkutano wa Mwaka 5 waTEHAMA unaendelea katika Kituo Cha Kimataifa Cha Mikutano AICC Jijini Arusha

Neema Lugangira Mbunge wa viti Maalum CCM ambaye anawakilisha Asasi za Kiraia NGO kutoka Tanzania Bara akizungumza anwandishi wa habari katika Mkutano wa tano Mwaka unaendelea Jijini Arusha
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...