Na John Walter-Manyara

Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Simon Sirro amewaagiza viongozi katika kila mtaa na vijiji kuhakikisha kunakuwepo na ulinzi ili kuziba mianya ya uhalifu.

Aidha amewataka viongozi hao kuanzia ngazi ya kata kutoa ushirikiano kwa makamanda wa jeshi la polisi ili kutatua changamoto za kiusalama zilizopo katika maeneo hayo.

IGP Sirro ameyasema hayo Oktoba 6,202 alipokutana na wazee maarufu,viongozi wa dini,watendaji wa mitaa,vijiji,kata na wenyeviti mkoa wa Manyara.

Kwa upande mwingine kiongozi huyo wa jeshi la polisi hapa nchini amewataka wazazi kuwaripoti watoto wao ambao ni wahalifu ili waweze kusaidiwa kuachana na tabia hizo.

“Leta taarifa tukusaidie, na taarifa sio kumfunga tu, wewe unae mtoto wako jambazi au unaona anao uelekeo wa ujambazi,anayo silaa,leta taarifa polisi tutajua namna ya kumrekebisha” alisema IGP Sirro.




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...