Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amewataka askari wa Jeshi hilo kutimiza wajibu wao ili kuweza kukabiliana na matukio ya uhalifu na wahalifu pamoja na vitendo vingine vya uvunjifu wa amani vinavyojitokeza kwenye jamii.
IGP Sirro amesema hayo leo wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya Medani za kivita katika kambi ya Kambapori iliyopo West Kilimanjaro katika wilaya ya Siha ambapo askari wa kozi ya cheo cha Mkaguzi Msaidizi wa Polisi kesho tarehe 08 Oktoba 2021 wanatarajia kuhitimu mafunzo yao ya miezi minne na kupanda cheo cha Mkaguzi Msaidizi wa Polisi katika Shule ya Polisi Moshi.
Naye Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Khamis Chilo amesema kuwa, Rais wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa ya kupandisha vyeo hasa kwenye Vyombo vya Ulinzi na Usalama ambapo Mheshimiwa Chilo pia amewataka askari Polisi kwenda kutimiza wajibu wao katika kuhakikisha usalama wa raia na mali zao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...