Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya sunny safaris Firoz suleman akipata chanjo
 Mkazi Arusha akipata chanjo,Viola Mfuko   


Na.Vero Ignatus,Arusha

Mkoa wa Arusha ,umetangaza mkakati kuwafuata majumbani na Kupitia viongozi jamii za kifugaji ili kupata elimu ya chanjo ya Uviko-19 baada ya jamii hizo kuwa nyuma katika awamu ya kwanza.

Mratibu wa chanjo ya Uviko-19 Mkoa Arusha Dkt. Willson Boniface amesema wilaya za Ngorongoro na Longido zipo nyuma katika chanjo awamu ya kwanza sasa mkazo wa umeongezwa katika elimu.

Hata hivyo amesema Mkoa katika awamu ya kwanza uliofanya vizuri kwa kuchanja 47,950 kati ya Chanjo 50,000 zilizopokelewa.

 Mratibu wa chanjo ya Uviko-19 mkoa Arusha Dkt. Willson Boniface amesema zoezi la Chanjo awamu ya pili limeanza na wanatarajia Wakazi wengi kujitokeza.

Amesema katika awamu ya kwanza, Jiji la Arusha ndio limeongoza Kwa kuchanja watu wengi zaidi likifatiwa na Halmashauri ya Arusha Dc na Halmashauri ya Meru..

Amesema awamu ya kwanza jamii za kifugaji zilikuwa  nyuma kutokana  na upotoshwaji uliokuwepo ,lakini Sasa hali imeanza kuwa tofauti kutokana na elimu inayotolewa majumbani,Kwa viongozi wa Mila na makanisani.

Mwisho

Amesema Mkoa Arusha tayari umepokea chanjo nyingine 39,809 aina ya sinopharm ambazo mtu atapata chanjo Mara mbili.

"Baada ya kupokea chanjo za pili aina ya sinopharm Sasa elimu tunaendelea kutoa na watu wameendelea kuchanja"amesema

Amesema katika awamu ya pili watu watapata chanjo mara mbili tofauti na chanjo ya awamu ya kwanza ya Johnson & Johnson

" Tunaomba watu wajitokeze kwani chanjo zipo salama kabisa na safari hii chanjo itakuwa ni mara mbili"amesema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...