Mwandishi wetu, Arusha
WAFANYAKAZI zaidi ya 2000 katika mashamba ya Maua Saba yaliyofungwa kutokana na changamoto mbalimbali ikiwepo ugonjwa ya Uviko-19 waimeomba Serikali kuwasaidia kupata mafao Yao zaidi ya Sh.bilioni tatu.
Mashamba makubwa Saba ya maua Saba yamefungwa kutokana na changamoto za athari za Uviko-19 katika nchi za Ulaya kutokana na kupungua wateja wa Maua na changamoto za Uwekezaji.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi,baadhi ya wafanyakazi hao kutoka shamba la Kili Flora na Shamba la Mount Meru,wameomba Serikali kusaidia walipwe stahiki zao na kutafuta wawekezaji wengine kujua mashamba hayo Kwa maslahi mapana ya Taifa.
Jane laizer alisema katika Shamba la kili flora wa lililokufa wapo zaidi ya ya wafanyakazi 500 wanadai zaidi ya sh.bilioni 3 .1."Shamba kimefungwa hatujuwi hatma yetu,tunaomba serikali kusaidia tulipwe."
Mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi katika shamba la Mount Meru,Hamza Seleman amesema wanaomba Serikali kusaidia walipwe na kumrejesha mwekezaji aliyeondoka katika Shamba hilo.
Amesema wanadai mishahara zaidi ya Sh.milioni 300 na kwa hali ilivyo sasa hawaoni kama watalipwa kwa shamba halina uzalishaji na soko la nje limeathiriwa na uviko-19.
Mkurugenzi wa Shamba hilo, Lucy Urio alikiri wafanyakazi hao kushindwa kulipwa mishahara na stahili zao tangu mwezi octoba mwaka 2019 kutokana na migogoro kadhaa ikiwepo ya uendeshaji na kuathirika biashara ya maua kutokana na ugonjwa wa uviko-19 duniani.
Amesema wafanyakazi wanadai zaidi ya sh 300 milioni , mfuko wa hifadhi ya jamii wa NSSF unadai sh 700 milioni pia ana mikopo mingine na kodi zaidi ya Sh.bilioni 25.
Wafanyakazi hao hivi karibuni walifika na kabango katika mkutano wa Rais Samia Suluhu katika eneo la chekereni wilayani Arumeru ambapo baada ya kusoma aliahidi serikali kufatilia Mgogoro huo.
Rais alisema Serikali itahakikisha wanalipa stahiki zao lakini pia kutafutwa wawekezaji wengine.
Mtendaji Mkuu chama cha Wakulima wa Maua na mbogamboga nchini(TAHA) Dkt.Jacqueline Mkindi anasema sekta hiyo ilikuwa inakuja kwa kasi na ilifikia asilimia 11 kwa mwaka lakini kutokana na janga la UVIKO-19 imeshuka na kufikia asilimia 7 pamoja na maeneo mengine ambayo hayafanyi vizuri Kama kufa kwa mashamba ya maua.
Aliomba Serikali kufuta madeni ambayo mashamba yaliyokufa yanadaiwa na kuweza kuwapa wawekezaji wapya nafasi ya kuwekeza kwani mashamba hayo yalikuwa yanaingiza fedha nyingi pamoja na kutoa ajira kwa watanzania.
,Naibu waziri wa Kilimo ,Hussein Bashe ameagiza ofisi ya Mkuu wa mkoa Arusha na wilaya Arumeru kuharakisha mikakati ya ufufuaji wa mashamba saba yaliyosimamisha uzalishaji maua,mboga na matumda ili kuongeza ajira na mapato serikali.
"Kwa kufufua mashamba haya yatasaidia kuongeza ajira na kuwasaidia vijana na wanawake katika kujikwamua kiuchumi na kutoka katika hali ya umasikini kwani mazao haya ni ya kisasa na yanajiuza kwa njia mbalimbali ikiwemo mitandaoni na Serikali imeweka nguvu katika kuhakikisha wakulima wa mazao ya horticulture wanapata masoko hasa ya Kimataifa,"amesema.
Wakati huo huo Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mhandisi Richard Ruyango amesema tayari Serikali imepokea kero ya wafanyakazi wa mashamba hayo yaliyopo wilaya ya Arumeru.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...