Na.Khadija Seif, Michuzi Tv
MASHINDANO ya kucheza Muziki kwa vikundi pamoja na mtu Mmoja mmoja hapa nchini (Furaha dance) yanatarajiwa kufikia tamati katika ukumbi wa Jangwani Sea breeze jijini Dar es salaam.
Akizungumza na Michuzi Tv, Muandaaji wa Shindano Hilo Furaha Dominick amesema kupitia Mchakato ambao ulijumuisha Mikoa mbalimbali ikiwemo Mbeya,Dodoma,Mbeya,Mwanza na kisiwa Cha zanzibar waliweza kupata wawakilishi ambao walifanikiwa kuingia kwenye mchujo Hadi kufikia Fainali ya kuisaka zawadi ya Milioni 10.
"Timu nzima ya Fdt iliweza kuzunguka Mikoani kwa ajili ya kuwapata wawakilishi wa kuingia Kwenye Mchujo na hatimae kutinga Fainali na kuhakikisha wanafika Dar es salaam kuendelea na fainali"
Aidha,Dominick ameeleza kwa namna gani kulikuwepo na ushindani mkubwa wa kupatikana kwa Washiriki hao.
"Mchakato ulikua wa haki na wazi kutokana na kuwepo wabobezi ambao wapo katika Sekta hiyo ya utumbuizaji hivyo kwa upande wa kutafuta Washiriki Bora haikuwa na ugumu Sana japo wengi walionyesha juhudi zao na kila kundi kuonekana Bora zaidi ya mwezie"
Pia amesema Kilele cha Fainali hiyo itafanyika octoba 23 mwaka huu katika ukumbi wa Jangwani Sea breeze uliopo Mbezi beach jijini Dar es salaam na kusindikizwa na wasanii mbalimbali.
"Fainali hiyo itakwenda sambamba na Burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii wa nyumbani akiwemo Jay Melody,Sholo Mwamba,Man fongo,Makomando na wengine wengi."
Muandaaji wa Shindano la kucheza (FDT) Furaha Dominick akizungumza na Waandishi Wahabari na kutangaza rasmi Fainali ya Shindano Hilo litakalofanyika octoba 23 mwaka huu Katika ukumbi wa jangwani sea breeze jijini Dar es salaam
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...