Na
Bartholomew Wandi
Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ikionozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo,
Mhe. Nagy Kaboyoka, leo tarehe 23/10/2021 imetembelea Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC) kujiona Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Tume ya
Taifa ya Uchaguzi katika eneo la Njedengwa Jijini Dodoma.
Kamati hiyo
ya Bunge kwa pamoja imefurahishwa sana na mradi wa Ujenzi wa Ofisi hizo za Tume
zilizoko katika eneo la Njedengwa Jijini Dodoma.
Ambao kwa asilimia kubwa umekamilika.
Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera Charles
akiielezea Kamati hiyo kabla ya kuitembeza kwenye Ofisi za Tume na maandhali ya
kuvutia ya nje, alisema kuwa ofisi za Tume zina
Majengo matatu ambayo ni Jengo la Utawala (Main Building), Jengo la Kuhifadhia
Vifaa (Warehouse) na Jengo la kutangazia matokeo (Results Center)
Mkurugenzi alifafanuwa kuwa kwa ujumla ujenzi wa majengo yote matatu unaendelea
vizuri kwani majengo yako katika hatua mbalimbali ambapo hadi sasa Jengo la Utawala limekamilika kwa
asilimia 99 na makabidhiano ya awali yalifanyika tarehe 22 Julai, 2020, Jengo
la Kuhifadhia Vifaa asilimia 99 na Jengo la kutangazia matokeo kwa asilimia 97.
Aidha, Mkurugenzi aliielezea Kamati hiyo ya Bunge kuwa Jengo la Utawala na
Jengo la Kuhifadhia Vifaa yameshaanza kutumika na inaendelea na ukamilishaji wa
shughuli nyingine zinazotekelezwa na wazabuni mbalimbali.
“Tume inaishukuru serikali kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa ofisi
hizi na hivyo kufanikisha Tume kuwa na majengo yake Dodoma na kwa ujumla,
ujenzi wa majengo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi unaelekea kukamilika kwani
umeshafikia hatua ya kumalizia shughuli ndogondogo ambazo zinatarajiwa
kukamilika ifikapo Oktoba 30, 2021 na hadi sasa mradi huu umegharimu jumla ya kiasi cha
Shilingi 19,713,413,335.44 “ Alisema
Mkurugenzi wa Uchaguzi
Pamoja na hayo, Mkurugenzi wa Uchaguzi aliielezea Kamati
ya Bunge kuwa Tume ina uhitaji wa Ujenzi
wa ofisi ndogo Jijini Dar es Salaam katika eneo lake lililopo Garden Avenue.
Mkurugenzi alifafanua kuwa ni muhimu kuwa na ofisi ndogo
Dar-es-Salaam kwakuwa Tume inafanya kazi na wadau wengi ambao bado wapo
Dar-es-Salaam na vifaa vingi vya uchaguzi huwa vinashushwa katika bandari ya
Dar-es-Salaam.
Zaidi ya hayo, Charles alisema kuwa Tume inauhitaji wa
kutatafuta eneo lililokaribu na reli ya SGR ili kujenga maghala mengine Dodoma
kwa ajili ya kuiwezesha Tume kuhifadhi vifaa vyake vyote.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Nagy Kaboyoka,
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...