Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo ameitaka serikali kuendelea kujenga mabweni katika wilaya ya Longido ikiwa ni mkakati wa kuiinua wilaya hiyo katika sekta ya elimu kutokana na umbali uliopo kati ya kijiji kimoja na kingine unaokadiriwa kuwa ni wastani wa kilometa 60 na uwepo wa wanyama wakali.

Katibu Mkuu Ndg. Chongolo ametoa maelekezo hayo leo tarehe 18 Oktoba, 2021 katika ziara ya kikazi ya Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Mhe. Samia Suluhu Hassan Mkoani Arusha wilayani Longido.

Katibu Mkuu Ndg. Chongolo akifafanua maelekezo hayo, ameeleza kuwa, kuna shule ya msingi ipo kijiji cha Irichang'isapukini kata ya Gerairungwa wilayani Longido, iliyopo umbali wa kilometa 130 kutoka Makao Makuu ya Wilaya, imeshakamilika kujengwa na mabweni yameshajengwa, wananchi wanasubiri idhini kutoka serikalini ili iingizwe kwenye bajeti ya shule za bweni.

Hivyo, Katibu Mkuu Ndg. Chongolo, ameitaka Serikali kuharakisha kuiingiza shule hiyo kwenye mpango wa bajeti wa shule za bweni, ili ianze kupokea wanafunzi wa bweni kama inavyofanyika katika shule za msingi za  Sinya, Longido na Ketumbeine ambapo zote hizi zinahudumiwa na serikali kwa asilimia 100.

Aidha, katika hatua nyingine, Katibu Mkuu Ndg. Chongolo kwa niaba ya WanaLongido na Chama Cha Mapinduzi, amemshukuru Mhe. Rais Samia kwa uamuzi wa kumalizia ujenzi wa kipande cha barabara chenye kilometa 44 kwa kiwango cha lami kutoka Ererai mpaka Kamwanga kupitia maeneo ya ormorog, Lelang'wa, Irkaswa, Kitendedi na maeneo mengine, ambapo kipande hicho kitakamilisha barabara ya mzunguko (Ringroad) kuuzunguka Mlima Kilimanjaro.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...