Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh.Anthony Mavunde kwa kushirikiana na wananchi  ameanzisha ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari ya Mkoyo ikiwa ni sehemu ya mkakati wake wa kuboresha sekta ya Elimu katika Jimbo la Dodoma Mjini.

Mbunge Mavunde ameshiriki katika zoezi la uchimbaji msingi wa madarasa na kutumia fursa hiyo kuwashukuru wananchi wa Hombolo Mkoyo kwa kujitolea nguvukazi ili kufanikisha zoezi hilo ambapo Shule hii ikikamilika itawapunguzia mwendo wanafunzi wa Mkoyo wanaotembea kilomita  9 kufuata Shule ya Sekondari Hombolo Bwawani.

Katika kuanzisha mchakato wa ujenzi huo wa ujenzi wa madarasa kwa ajili ya Sekondari Mbunge Mavunde amechangia kokoto,saruji mifuko 100 na matofali 2000.

Aidha zoezi hilo lilitanguliwa na ukaguzi wa ujenzi wa Shule ya Msingi Ngh’ole ambapo Mbunge Mavunde alichangia matofali 1000 na saruji mifuko 80 pamoja Shule Mpya ya Ndachi ambapo pia amechangia matofali 2000 na saruji mifuko 130.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi Diwani wa kata ya Hombolo Bwawani Mh Assed Ndajilo amemshukuru Mbunge Mavunde kwa namna ambavyo amekuwa chachu ya maendeleo katika kata ya Hombolo Bwawani na kuahidi kuendelea kumpa ushirikiano ili kukamilisha miradi yote aliyoianzisha.

 










 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...