Charles James, Michuzi TV

UMOJA wa Wanawake Tanzania (UWT) umesema kuwa katika kuiboresha Jumuiya yao na kuifanya kwenda kisasa tayari imeanza ujenzi wa Ofisi za Makao Makuu ya Jumuiya hiyo jijini Dodoma ambazo zitagharimu kiasi cha Sh Milioni 378 Hadi kukamilika kwake.

UWT imesema ujenzi huo umelenga kuifanya Jumuiya hiyo kuondoka katika majengo ya Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambapo kwa sasa ndio wanayotumia kwa shughuli zao na kwamba ujenzi huo utawawezesha kuwa na Ofisi zao wenyewe kwa ajili ya viongozi na watumishi sambamba na ukumbi wa mikutano utakaokua na uwezo wa kubeba watu 200 kwa wakati mmoja.

Akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya Wiki ya UWT kitaifa Wilayani Rufiji mkoani Pwani, Mwenyekiti wa UWT Taifa, Gaudentia Kabaka amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kukubali kuwa mgeni rasmi katika kilele hicho na kwamba yeye ndie Bibi Titi Mohamed mpya wa Tanzania.

Amesema maadhimisho hayo yamefanyika Rufiji kama sehemu pia ya kumuenzi Bibi Titi Mohamed kwa Mchango wake mkubwa katika harakati za kudai Uhuru wa Tanganyika akifanya kazi kwa karibu na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.

" Bibi Titi ndie muasisi wa Jumuiya yetu hii na Mwenyekiti wa kwanza wa UWT Taifa, lakini pia alipata bahati ya kuwa Mbunge wa kwanza mwanamke wa Jimbo hili la Rufiji kwetu sisi ni heshima kusherehekea maadhimisho haya hapa kwake.

Niseme tu kwa sasa tunae Bibi Titi Mohamed mwingine ambaye ni wewe Rais Samia Suluhu Hassan, umeweka rekodi ya kuwa Rais wa kwanza Mwanamke na Mwenyekiti wa Chama chetu, kazi yako iliyotukuka ndani ya miezi michache ya uongozi wako ni kubwa na sisi tuna imani na wewe," Amesema Kabaka.

Awali Katibu Mkuu wa UWT, Dk Philis Nyimbi amesema Jumuiya hiyo itaendelea kushirikiana na Serikali katika kuboresha maisha ya Wanawake nchini ikiwemo kuhakikisha wanajiinua kiuchumi.

Amesema kuelekea maadhimisho ya kilele hicho leo kwa siku ya jana UWT ikiongozwa na Mwenyekiti wake Kabaka ilitembelea maeneo mbalimbali ya kijamii na kutoa mchango wao.

" Jana tulitembelea Shule ya Sekondari ya Utete na kugawa taulo za kike, Hospitali ya Wilaya ya Rufiji ambapo tuligawa mashuka kwa ajili ya wagonjwa sambamba na kituo cha watoto yatima ambao tuliwapelekea mahitaji mbalimbali," Amesema Dk Nyimbi.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...