Na Amiri Kilagalila,Njombe
Jeshi la polisi wilaya ya Ludewa mkoani Njombe limepokea msaada wa tairi tano kwa ajili ya kufunga kwenye vyombo vyao vya usafiri ili kuongeza ufanisi wa vikosi kazi vya jeshi hilo vinapohitajika kufika katika maeneo mbali mbali kwa ajili ya operation.
Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo kutoka kwa shirika la Rafiki Foundation la mjini Njombe,mrakibu wa jeshi la polisi na kaimu mkuu wa jeshi hilo wilaya ya Ludewa Super litendent Hussein Gawile ameshukuru kwa msaada huo utakao ongeza chachu ya ufanisi katika kazi.
“Tuna uthamini sana msaada wenu mlioutoa kwa jeshi la polisi na tunaamini kabisa hii ni chachu itakayoongeza ufanisi katika utendaji wa kazi”alisema Gawile
Vile vile ametoa wito kwa wengine wenye nia na mapenzi ya kulisaidia jeshi hilo kuto kusita na kuiga mfano ili jeshi hilo lizidi kuwa imara na kuwatumika wananchi kikamilifu.
“Tunaomba na kwa wengine ambao watakuwa na nia ya kulisaidia jeshi la polisi basi wasisite na waige mfano huu kwa kuwa ni mzuri”aliongeza Gawile
Rosalia Johnbosco Mgeni amekabidhi msaada huo kwa niaba ya mkurugenzi wa shirika la Rafiki Foundation na kubainisha kuwa wamewiwa kutoa msaada huo kutokana na kuridhishwa na utendaji kazi wa jeshi.
“Tumeridhishwa na utendaji kazi wa jeshi la polisi wilaya ya Ludewa kwa hiyo tumeona tutoe fadhira zetu kwa kukabidhi matairi matano ili yaweze kusaiidia katika utendaji wao wa kazi wakati gari lao linapohitajika”alisema Rosalia Johnbosco Mgeni
Kwa mujibu wa muwakilishi wa shirika hilo Bi, Rosalia Johnbosco Mgeni amesema tairi hizo zimegharimu kiasi cha shilingi milioni mbili na laki tano.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...