Na Khadija Kalili, Kibaha
Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linamshikilia mtu mmoja Abdul Selemani (27), kabila Mluguru mfanyabiashara ya Stationary mkazi wa Visiga kwa kipofu, Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani kwa kosa kutengeneza nyara za Serikali.
Akizungumza na Waandishi wa habari Leo Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani RPC Wankyo Nyigesa alisema kuwa tarehe 12.10.2021 majira ya saa 11:38 jioni katika eneo la Visiga kwa Kipofu Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola walimkamata mtuhumiwa huyo kwa kosa la kutengeneza na kuuza vitambulisho vya Taifa vya NIDA na kuviuza Tsh 10,000/- kwa kila kitambulisho kimoja anachotengeneza.
RPC Wankyo alivitaja vifaa mbalimbali alivyokuwa anatumia kuwa ni Vitambulisho viwili vya Taifa vya NIDA, komputa mpakato, Pvc card, Desktop Computer, Monitor, Frash Disk na Printer.
Aidha mtuhumiwa huyo atafikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.
Wakati huohuo alimtaja mtuhumiwa mwingine anyedauwa kutapeli watu mbalimbali aliyemtaja kwa jina la Peter Baziro ambaye pia hutumia la Pius Jaulos Nducha alikamatwa 14/10/2021 majira ya saa 10:00 jioni huko kwa mfipa, Wilaya ya Kibaha mkoa wa Pwani, Peter kwa kuwatapeli watu mbalimbali kwa kuwauzia viwanja na kughushi hati za viwanja anavyoviuza na hati za mauzo.
"Pia amekuwa akitapeli watu na kujipatia fedha kwa kuwauzia magari, mpaka anakamatwa amejipatia pesa kutoka kwa watu mbalimbali akiwemo Bi Jenifa Asa aliyemlipa mtuhumiwa kiasi cha Mil.4 kwa lengo la kumuuzia eneo la ukubwa wa 20 kwa 20 huku akijua kwamba siyo
kweli na hana eneo hilo.
RPC Wankyo alisema kuwa mtuhumiwa huyu amekuwa akibadilisha majina kila anapofanya tukio la kutapeli mtu ili asikamatwe. Baada ya mahojiano mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.
Alisema kuwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linaomba mtu yeyote aliyewahi kutapeliwa na mtu huyu afike kituo cha Polisi kibaha mji kwa utambuzi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...