RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Marehemu John Pombe Magufuli, alipofika nyumbani kwa marehemu kusalimia familia ya marehemu Chato na (kushoto) Mjane wa Marehemu Mama Janeth Magufuli na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi.


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akitowa salamu za heshima baada ya kuweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Marehemu John Pombe Magufuli alipofika nyumbani kwa marehemu Chato kusalimia familia ya marehemu na (kushoto) Mjane wa Marehemu Mama Janeth Magufuli na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi.(Picha na Ikulu)






RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge, Uratibu Kazi Ajira Vijana na Wenye Ulemavu Mhe Jenista Joakim Mhagama,wakimsikiliza Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Kanda Chato Dr.Marygoreth Changaluda alipotembelea alipotembelea mabanda ya Maonesho ya Wiki ya Vijana yanayofanyika katika viwanja vya Mazaina Chato.


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakimsikiliza Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Zanzibar Ndg. Yussuf Juma akitowa maelezo ya bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na Mabaraza ya Vijana Zanzibar, wakati alipotembelea banda lao katika maonesho ya Wiki ya Vijana yaliofanyika katika viwanja vya Mazaina Chato Mkoani Geita.




WANANCHI wa Chato Mkoani Geita wakishangilia wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayuko pichani) akiwahutubia katika viwanja vya Mazaina Chato baada ya kutembelea Maonesho ya Wiki ya Vijana yaliofanyika katika viwanja hivyo.ikiwa ni shamrashamra za Kilele cha Mbio za Mwenye wa Uhuru na Kumbukizi wa Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.


WASANII wa Kikundi cha Taraab cha Wajelajela wakitowa burudani katika viwanja vya Mazaina Chato wakati wa maonesho ya Wiki ya Vijana yaliofanyika katika viwanja hivyo.

 

WANANCHI wa Chato Mkoani Geita wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akiwahutubia katika viwanja vya mazaina Chato, baada ya kutembelea Maonesho ya Wiki ya Vijana yaliofanyika katika viwanja hivyo.

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwahutubia Wananchi wa Chato Mkoani Geita katika viwanja vya Mazaina, baada ya kutembelea maonesho ya Wiki ya Vijana yaliofanyika katika viwanja hivyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...