Membe amempongeza Rais Samia kwa kazi kubwa anayoifanya na ameahidi kumuunga mkono katika jitihada za kuwaletea watanzania maendeleo.Membe ameongeza kuwa Rais Samia ni kiongozi mahiri, jasiri na anatosha kuiongoza Tanzania.
WAZIRI Mstaafu wa Mambo ya Nje, Bernard Membe amesema Rais Samia Suluhu Hassan ni kiongozi jasiri na mahiri, anatosha kuiongoza Tanzania na anamuunga mkono kwa kazi kubwa anayoifanya.
Membe ameyasema hayo leo (Jumanne 5 Octoba 2020) alipozungumza mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ambaye yuko katika ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo Mkoani Lindi.
Membe amemuomba Waziri Mkuu afikishe salamu zake pamoja na za wananchi wa kijiji cha Rondo kwa Mheshimiwa Rais Samia kwamba wanamuunga mkono katika jitihada kubwa za kuwaletea wananchi maendeleo.
“Mheshimiwa Waziri Mkuu naomba ufikishe salamu zetu sisi Wana-Rondo kwa Mheshimiwa Rais Samia mwambie tunampenda, anatosha na tutamsaidia,” Amesema Membe.
Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Rondo, Waziri Mkuu amewasihi wananchi hao wawapeleke watoto shule, kuanzia ngazi ya elimu ya awali na shule za Sekondari kwani Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na mama Samia Suluhu Hassan imeweka msisitizo katika kuhakikisha kila Mtanzania anapata elimu bora.
Aidha, Waziri Mkuu ametoa onyo kali kwa vijana na watu ambao wamekuwa wakiwarubuni wanafunzi wa kike kuacha masomo na wengine kuwapa mimba waache ili watoto hao waweze kutimiza ndoto zao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...