Na Khadija Kalili Kibaha

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Samia Suluhu Hassan  atakuwa mgeni  rasmi  katika kilele cha  maadhimisho  ya Jumuiya ya  Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi  (UWT ) yatakayoadhimishwa kitaifa  Rufiji Mkoani Pwani.

Menyekiti wa  UWT Taifa  Gaudencia Kabaka amesema hayo leo alipozungumza na Waandishi wa habari Kibaha Mkoani Pwani alisema  Rais Samia Suluhu  ataungana na wanawake  zaidi ya 700 ambapo alifafanua kuwa wanawake 500 tayari wamethibutisha kushiriki katika kilele hicho.

Aliongeza kwa kusema kuwa lengo la kupeleka sherehe hizo  za maadhimisho  ya wiki ya UWT Rufiji ni katika kumuenzi aliyekuwa muasisi wa UWT Taifa Hayati Bibi Titi Mohamed ambaye pia alikua Mwanachama mwenye kadi namba 16 ya chama.
 
Kabla kufikia kilele hicho  Oktoka 23 kesho Ijumaa UWT Taifa wakiongozwa na Mwenyekiti Taifa Mama Kabaka watakwenda kutoa misaada katika Shule za Sekondari za wasichana ikiwemo Ikwiriri,  watafanya usafi,  na kutoa mahitaji ya wasichana , pia watatembelea  katika hospitali mbalimbali ambapo watatoka mashuka ambayo yatawekwa  na sabuni.

"Misaada hii itakuwa ni kumbukumbu yetu kwao kwa kumkumbuka muasisi wa UWT Hayati bibi Titi Mohammed ambaye ni mazaliwa wa Rufiji"alisema Kabaka.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani   Alhaj Abubakari Kunenge amewashukuru UWT Taifa kwa kufanya maamuzi ya kupeleka sherehe hizo Wilayani Rufiji kwani itachangia kutangaza Mkoa wa Pwani na kutangaza katika fursa za kitalii kwa ujumla.
"Pia tunamshkuru sherehe hizo zitaiifungua Wilaya ya Rufiji na Mkoa wa Pwani kufahamika ambapo Mkoa uko katika mkakati wa kuifungua vivutio vilivyopo eneo hilo, namshkuru pia Rais Samia Suluhu Hassan kwa jinsi anavyopigania ustawi wa maisha ya wananchi wote" alisema RC Kunenge.
 Naye Katibu w UWT Taifa  Dkt. Philis Nyimbi (MNEC) , alisema kuwa hivi Sasa UWT wanawachama zaidi ya Mil.2.4 na bado wanaendelea kuwatambua kidijitali.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...