Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Ujumbe wa Wadhamini wa Tamasha la Sea Food Festival linalotarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii katika Mkoa wa Kaskazini Unguja na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe.Ayoub Mohammed Mahmoud na (kushoto kwa Rais) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said na Afisa Mkuu wa Ukaguzi wa Ndani wa Benki ya NMB.Bw.Benedicto Baragomwa, mazungumzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuagana na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja.Mhe.Ayoub Mohammed Mahmoud, baada ya kupokea taarifa ya kukamilika kwa maandalizi ya Tamasha la Sea Food Festival linalotarajiwa kufanyika katika Mkoa wa Kaskazini Unguja mwishoni mwa wiki hii.(Picha na Ikulu)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...