- Asema eneo hilo halifai kwa makazi.
- Awataka Wananchi wa eneo husika kuchukuwa tahadhari.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amelitangaza eneo la Kunduchi lenye Volcano ya Tope kuwa eneo la hatari na halifai kwa makazi na kuwataka Wananchi wa familia Tisa ambazo makazi yao yameathiriwa kuanza kuchukuwa tahadhari.
RC Makalla amesema hayo alipotembelea na kukagua eneo hilo kujionea athari za Volcano hiyo na kulielekeza Jeshi la Polisi kuweka uangalizi Katika eneo hilo.
Aidha RC Makalla amesema taarifa ya kitaalamu iliyowasilishwa ofisini kwake inaeleza kuwa eneo hilo halifai kwa makazi ndio maana amefika kuwataka kuchukuwa tahadhari wakati Serikali inaangalia hatua za kuchukuwa.
Pamoja na hayo RC Makalla ameelekeza eneo hilo kuwekewa alama za tahadhari ili kuwaepusha wananchi na maafa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...