Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Adam Malima (katikati) akizungumza na Kanali Khaji Mtengela (kulia kwake) akifuatiwa na Kanali Karimu Machake kutoka Chuo Ukamanda na Unadhimu Duluti, kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Pili Mnyema.
Wakuu wameongoza ujumbe wa wanafunzi 53 wa Kozi ya Ukamanda na Unadhimu kwa ajili ya ziara ya kimafunzo ndani ya nchi jijini Tanga.
Wakiwa mkoani Tanga, wanafunzi hao kutoka nchi mbalimbali, watatembelea viwanda kikiwamo Kiwanda cha Saruji (Tanga Cement) na Kiwanda cha Maziwa (Tanga Fresh), Bandari ya Tanga na Bodi ya Mkonge ili kujionea mambo mbalimbali ikiwa ni sehemu ya mafunzo yao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...