Na Amiri Kilagalila,Dodoma

Serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia wizara ya kilimo inatarajia kuunda kitengo maalum kitakachokuwa na jukumu la kushughulikia maswala ya kilimo hai pamoja na kukitengea fedha ili kuongeza jitihada na ufanisi wa kilimo hicho.

Hayo yamebainishwa na naibu waziri wa kilimo Mhe.Hussein Mohamed Bashe (Mb) wakati akifungua kongamano la pili la kuchaguza kuelekea kwenye kilimo endelevu ili kufikia katika hatua za upatikanaji wa chakula lilifonyika katika ukumbi wa mikutano wa St.Gaspar uliopo mkoani Dodoma.

Bashe amebainisha kuwa miongoni mwa sababu za kukipa kipaumbele kilimo hicho ni pamoja na sababu za kiafya ili kupunguza ghalama za matibu kwa wananchi,kuongeza thamani ya mazao pamoja na utunzaji wa mazingira.

“Hatutakuwa na dawati,tutakuwa kitengo kinachoshughulika na swala la kilimo hai na tutaanza kukitengea fedha kwenye bajeti ya mwaka 2022-2023”alisema Waziri Bashe

Aidha amesema wizara inatarajia kuanzisha benki kubwa ya mbegu za asili ili kurahisisha upatikanaji wa mbegu kwa ajili ya kilimo hai.

“Wizara tutaanzisha benki kubwa ya mbegu za asili kwa kuwa wala hatuhitaji vitu vingi sana kuumiza kichwa,tunahitaji jengo na washirika wetu hapa wapo wakutusapoti,tuna majengo mengi pale nane nane,Kwa hiyo tutatafuta jengo letu moja la kuanza kuhifadhi mbegu zetu za asili na tuanze mfumo wa kusafisha mbegu za asili na kuzirudisha mashambani”alisema Bashe
 
Kwa upande wake mkurugenzi wa mazao na pembejeo kutoka wizara ya kilimo Beatus Malema amesema kutokana na umuhimu wa pekee wa kilimo hicho katika maisha ya binadamu wiazara itaendelea kushirikiana na wadau mbali mbali ili kuendeleza zaidi kilimo hicho.

Nao baadhi ya wadau waliohudhuria katika kongamano hilo akiwemo mkuu wa mkoa wa Simiyo David Kafulila wameahidi kuendeleza kilimo hai.

“Hiki kilimo kinaweza kuja kuwa na mapinduzi makubwa,kama mkuu wa mkoa wa Simiyu ambao unaongoza kwa Pamba na pia kuongoza kwa hii Organic Coton ninayo kila sababu ya kusema mafunzo yatakayopatikana hapa tutayatumia kikamilifu kuhakikisha kwamba tunafanya mara dufu ya kiasi ambacho tunafaya sasa”alisema Kafulila
Naibu waziri wa Kilimo Hussein Bashe akizungumza na wadau mbali mbali katika kongamano la pili la kilimo endelevu lililofanyika mkoani Dodoma

Baadhi ya wadu washiriki wa kilimo hai wakimsikiliza waziri wa kilimo katika kongamano la pili lililofanyi mkoani Dodoma kwa lengo la kuendeleza kilimo hai nchini.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...