Waziri wa Mambo ya Nje, Biashara na Vivutio vya Kiuchumi wa Ufaransa, Mhe. Franck Riester akiongea na washiriki wa Kongamano lililowakutanisha Mawaziri wa Kisekta, wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Ufaransa Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiongea na washiriki wa Kongamano lililowakutanisha Mawaziri wa Kisekta, wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Ufaransa Jijini Dar es Salaam.



Mawaziri wa Kisekta pamoja na Wafanyabiashara na Wawekezaji kutoka Ufaransa wakiendelea na Kongamano Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje, Biashara na Vivutio vya Kiuchumi wa Ufaransa Mhe. Franck Riester akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kumalizika kwa Kongamano lililowakutanisha Mawaziri wa Kisekta, wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Ufaransa Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa Kongamano lililowakutanisha
Mawaziri wa Kisekta, wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Ufaransa Jijini Dar es Salaam.



TANZANIA imezihakikishia Kampuni za Kifaransa kuwa mazingira ya biashara na uwekezaji ni salama na kuwasihi kuwekeza kwa wingi hapa nchini.

Akiongea na Waandishi wa Habari mara baada ya kumalizika kwa kongamano lililowakutanisha Mawaziri wa Kisekta, wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Ufaransa Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) amesema Serikali imewahakikishia wafanyabishara na wawekezaji wa kampuni za Kifaransa kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inajenga na inaendelea kuboresha mazingira rafiki ya uwekezaji kwa kuondoa kero mbalimbali zilizokuwa zinawakabili wawekezaji hapa nchini.

“Serikali ya Awamu ya Sita iko serious….. na tuna azma kubwa ya kuhakikisha kwamba tunajenga mazingira rafiki ya kuweza kuwekeza na kuondoa kero zote ambazo zimekuwa zinajitokeza….na makampuni mengine yameeleza hizo kero lakini tunafurahi kuona kero hizo tayari zimeanza kuondolewa,” amesema Balozi Mulamula

Balozi Mulamula ameongeza kuwa Wafaransa wamekuwa na uhusiano mzuri na Tanzania kwa muda mrefu na hivi sasa wamekuwa na shauku ya kufanya biashara na kuwekeza kwa wingi hapa nchini…..ambapo takwimu zinaonesha watalii kutoka Ufaransa kuja Tanzania kila mwezi ni zaidi ya watalii 7000 wanaokuja kutembelea vivutio mbalimbali hapa nchini, hivyo ni changamoto kwetu kuchangamkia fursa hii adhimu.

Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya nje , Biashara na Vivutio vya Kigeni wa Ufaransa, Mhe. Franck Riester amesema Ufaransa inatambua jitihada zinazofanywa na Serikali ya Tanzania ikiwa ni pamoja na kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji mambo ambayo pia yanatiliwa mkazo na serikali ya Ufaransa.

“Ufaransa imedhamiria kuongeza ushirikiano na Tanzania na kama mlivyoshuhudia leo tumeanzisha safari za ndege za moja kwa moja kutoka Paris hadi Zanzibar ambao ulisimama tangu mwaka 1974, huu ni mwanzo mzuri” amesema Mhe. Riester

Mhe. Riester ameongeza kuwa wataendelea kuwaeleza na kuwahamasisha wafanyabiashara na wawekezaji wa Ufaransa juu ya fursa mbalimbali zinazopatika Tanzania ikiwemo katika sekta ya Nishati, Utalii, Viwanda, Usafirishaji pamoja na Uwekezaji ili kuja kuwekeza na kukuza ucbumi wa pande zote mbili.

Mawaziri wa Kisekta waliohudhuria kongamano hilo ni Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb), Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb), Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba (Mb) Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (Mb) Waziri wa Uwekezaji – Zanzibar Mhe. Mudrick Soraga, Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb) na Waziri wa Ofisi ya Rais Uwekezaji Mhe. Geoffrey Mwambe.

Kampuni zilizoshiriki katika kongamano hilo ni pamoja na; CMA-CGM, Bolloré, Airbus, Thales, Lagardére, Total, Chama cha Wafanyabiashara wa Ufaransa-Tanzania, Engie pamoja na Maurel & Prom.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...