KAMATI ya Mashindano ya MR Tanzania imesema wanatarajia kufanya shindano la Mr.Tanzania Oktoba 22,2021 na kwamba washiriki wote watatakiwa kuripoti katika ukumbi wa Kilimanjaro,Ubungo Plaza Dar es Salaam ya tarehe hiyo kuanzia saa moja asubuhi.
Akizungumza kuhusiana na shindano hilo leo Oktoba 13,2021 Katibu Mkuu wa Shirikisho la mchezo huo toka (TBBF ) Francis Mapugilo amesema wameamua kufanya shindano hilo pekee tu kwa mwaka huu kutokana na mdhamini kushindwa kumudu gharama za Mr Tanzania ,Mr Physique na Miss Fitness.
Amesema kamati imeomba radhi sana washiriki ambao vipengele vyao hivyo vitakosekana kutokana na sababu zilizonje ya uwezo wa kamati."Kwa watu waliotayari kugombea watalipa TSH.100,000(Shilingi Laki Moja tu) na hadi hadi sasa maandalizi kupelekea siku hiyo yanaendelea vizuri."
Mapugilo amesema fomu zinapatikana kwenye wavuti yao www.tzbbf.org katika safu ya usajili pia unaweza kuipakua kwa bure.
Ameongeza kuwa fomu pia zinapatikana katika kumbi za michezo mbali mbali Jijini Dar es Salaam maenei ya Gym Bodyline Mikocheni ,Gym Home Mwenge, Body Fuel Masaki pamoja na Gym zingine.
Kulekea shindano hilo wadau wa fani hiyo waliyoiona miaka tangu linaanza nchini wanasema hata fani ya urembo, Miss Tanzania ambayo kwa muda mwingi imekuwa ikiongoza kwa kuwa na wadhamini wengi, haikufua dafu mbele ya sanaa ya kutunisha misuli.
Pengine kama kuna mchezo uliwahi kupendwa zaidi katikati ya miaka ya 1990 ulikuwa ule wa kutunisha misuli.
Mchezo huu ulitajwa kila kona, ndiyo ulioongoza kuwa na wadhamini wengi kuliko fani nyingine yoyote ya burudani na michezo.
Hata fani ya urembo, Miss Tanzania ambayo kwa muda mwingi imekuwa ikiongoza kwa kuwa na wadhamini wengi, haikufua dafu mbele ya sanaa ya kutunisha misuli.
Isitoshe ni katika kipindi hicho kulifunguliwa vituo mbalimbali vya kunyanyua vitu vizito (Gym), huku pia kukiwa na mashindano kuanzia wilaya, mkoa mpaka taifa.
Mwasisi wa mashindano ya kutunisha misuli, Fike Wilson ndiyo haswa wanao urudisha mchezo huo katika chati.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Pilipili Intertainment Millesh Batt, ambao ndio waandaji washindano hilo amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi siku hiyo huku kwa wale ambao hawatobahatika kufika ukumbini.
"Uhakika ni hivi bodybuilding safari hii itakuwa ni (Free Class) kwa maana hakutakuwa na groups kutokana na uzito wao ."amesema Mapugilo.
Amesema wamefanya hivyo kutokana na ufinyu wa bajeti ya mashindano , na kutakuwa na kipengele cha best Poser ilikuleta ladha kwenye shindano .Zawadi kwa washindi zimetajwa kuwa ni kemkem ilikuchochea amasa katika shindano hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...