Kila ifikapo Oktoba 15 kila mwaka mamilioni ya watu duniani husherekea siku ya unawaji mikono kwa shughuli za aina tofauti. Siku hii hutumika kama kielelezo cha kukumbushana umuhimu wa kunawa mikono.
Tasisi ya MyLegacy kwa kushirikiana na Habitat for Humanity Tanzania leo imeadhimisha siku hiyo kwa jijini Dar es Salaam katika Shule ya Msingi Ukwamani na Soko la Kawe kwa kuikumbusha jamii umuhimu wa kunawa mikono ili kuleta tija kwa Taifa.
Akizungumza na wanafunzi Afisa Mradi wa Nawa Mikono kwa Afya, Boresha Makazi, Yasinta Mtavangu amesema jamii inapaswa kujenga utamaduni wa kunawa mikono kila mara ili kulipunguzia Taifa mzigo wa matibabu kwa magonjwa ambayo yangeweza kuepuka kwa kitendo cha kunawa mikono.
“Sio Serikali peke yake, hata jamii inaweza kujiepusha na gharama zisizo za lazima na kupoteza muda wakati wa kutafuta matibabu. Kunawa mikono kuna faida kubwa kwa jamii na Taifa kwa ujumla.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Fortunata Temu ameahidi kuwekeza nguvu katika kutoa elimu na vifaa vya kunawia mikono mpaka pale jamii yote itakapofanya unawaji mikono kuwa utamaduni.
Kupitia mradi wetu tulielimisha jamii na kupeleka vifaa vya kunawia mikono ambavyo baadhi ni matanki ya maji na sabuni.
“Katika kipindi cha miezi sita tuliwekeza katika kuelimisha na kutoa vifaa ambavyo vimehudumia watu 18,771, kati yao 10,262 wakiwa wanawake na wanaume 8,509. Malengo yetu yakiwa kupunguza kasi ya maambukizi ya ugonjwa wa UVIKO 19,” amesema Temu.
Jumla ya lita 3,500 za sabuni ya maji ziliwekwa katika vituo 35 vya kunawia mikono tulivyoweka katika shule nane, ofisi za kata, serikali za mitaa na masoko mawili.
Amesema vifaa 70 ikiwamo matanki ya kuhifadhia maji, sabuni za maji na ndoo viliwekwa katika shule, masoko na ofisi za serikali za mitaa.
Shule za sekondari wanufaika ni Kisauke , Twiga na Kondo Secondary Schools wakati shule za msingi ni Jangwani Beach, Ukwamani, Kawe, Wazo na Mtongani.
“Tunataka kuona unawaji mikono kila inapohitajika unakuwa utamaduni wa Mtanzania, ndio maana hatujawaacha nyuma wanafunzi na hii ni kuwaandaa kuwa raia wenye uelewa mpana wa umuhimu wa unawaji mikono,” amesema Temu.
Kwa miezi sita Taasis ya MyLegacy kwa ushirikiano na Taasisi ya Habitat for Humanity Tanzania imekuwa ikiendesha kampeni ya kunawa mikono ijulikanayo kama Nawa Mikono, Boresha Makazi.
"Kunawa mikono ni njia rahisi ya kuokoa maisha hasa ya watoto mashuleni kwa kuwakea vifaa rafiki ya kunawia mikono, lakini mlipuko wa ugonjwa UVIKO 19 unatuamsha katika umuhimu mara dufu wa mazoea haya,” amesema na kuongeza.
“Tunaweza kuukabili ugonjwa wa UVIKO 19, tunaweza kuyashinda magonjwa ya kuambukiza kwa kunawa mikono kwa maji safi yanayotiririka na sabuni.”
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...