TAASISI ya Bega kwa Bega na Mama kwa ushirikiano wa klabu za 'joging'za Dar es Salaama pamoja na waendesha pikipiki Mkoa wa Dar es Salaam wataungana na Umoja wa Wanawake wa Tanzania kwa ajili ya kufanya matembezi ya kumuenzi shujaa na mwanamama mzalendo Bibi Titi Mohamed.
Bibi Titi enzi za uhai wake ametoa mchango mkubwa katika Taifa na matembezi hayo yatazinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amoss Makalla na kisha kuelekea Wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani.
Mwana mama huyo ni mmoja wa viongozi ambo walionesha uzalendo wa hali ya juu katika Taifa hili huku ikielezwa kuwa Bibi Titi alikuwa miongoni mwa viongozi waliokuwa maarufu na mvuto kwa Watanzania, hivyo taasisi hiyo kwa kutambua mchango wake imeamua kuandaa matembezi kwa ajili ya kumuenzi.
Akizungumza leo Oktoba 18,2021 mkoani Dar es Salaam ,Katibu wa taasisi hiyo Fatma Suleiman Sarhan amesema matembezi hayo yatahusisha makundi ya watu wa rika mbalimbali,lengo ni kumuenzi mwanamama huyo shujaa na aliyefanya mambo makubwa yatalayokumbukwa kizazi na kizazi.
Amefafanua matembezi hayo yanatarajia kufanyika kesho Oktoba 19,2021 kuanzia saa moja asubuhi jijini Dar es Salaam na mgeni rasmi atakuwa Mkuu wa Mkoa.Vijana 3500 kati watashiriki na kati ya hao 500 watatoka mkoani Pwani kuungana na wenzao wa mkoa wa Dar es Salaam katika eneo la Kongowe mpakani mwa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.
Ameongeza baada ya kuondoka Kongowe, kutakuwa na vituo vitatu vya mapumziko,ambavyo ni vijiji vya Mwarusembe, Njopeka na Bungu ambapo itakuwa Oktoba 21 na 22 huku akisisitiza maatembezi hayo yataishia Ikwiriri wilayani Rufiji Oktoba 23 mwaka huu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa madereva wa bodobado nchini, Edward Mwinyisongele ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa wametambua umuhimu wa wao kushiriki kikamilifu katika matembezi hayo maalum ya kuenzi na kutambua mchango wa Bibi Titi.Lakini kutambua kazi kubwa na nzuri inayofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan tangu aingie madarakani kuongoza Watanzania."
Kwa kukumbusha tu Bibi Titi alifariki dunia Novemba 5 mwaka 2000 akiwa Afrika Kusini ambako alipelekwa kwa matibabu katika hospitali ya Net Care.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...