Na WAMJW Saint Petersburg Urusi
Tanzania imeazima kuendelea kuwawezesha wanawake katika nyanja mbalimbali ikiwemo katika Uongozi na uwezeshaji Wanawake Kiuchumi kupitia Majukwaa ya Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jinsia kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) Mwajuma Magwiza wakati akizungumza namna Tanzania ilivyojifunza kutokana na Mkutano huo wa Wanawake nchini Urusi.
Bi. Mwajuma amesema kuwa Tanzania imejifunza kuwa Wanawake wanaweza kushiriki katika Sekta mbalimbali na kutoa mchango wao katika Sekta husika na kutumia fursa hizo kupata ajira na kuajiri wengine.
Ameongeza kuwa Tanzania inahimiza Wanawake kushiriki katika uchumi wa viwanda ila kutokana na Mkutano huo imeleta changamoto mpya za kuangalia maneno ambayo Wanawake wanaweza kushiriki katika kupata fursa za kujikwamua kiuchumi na kuleta maendeleo.
Ameyataja maeneo hayo kuwa ni sanaa ya uigizaji, ulimbwende na michezo ambapo Wanawake wanaweza kushiriki vizuri iwapo kutakuwa na mazingira mazuri yanayoweza kuwa na tija katika maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.
"Katika Sekta hizi inabidi tuangalie ni maeneo yapi na yana changamoto gani kwa wanawake ili tuwasaidie waweze kufikia Kimataifa katika Sekta hizo" alisisitiza Bi Mwajuma
Aidha, ameongeza kuwa Tanzania imeshaanza na inaendelea kuwawezesha wanawake katika Uongozi na majukwaa ya Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi yameanzishwa katika ngazi za Wilaya na Mkoa ili kuweza kuwapa fursa katika Sekta mbalimbali.
"Nimejifunza kuwa katika kila eneo ambalo mwanamke anafanya kazi inatakiwa kupaangalia na kuona anachangamoto zipi na kumuwezesha ili aweze kujua Kitaifa na Kimataifa" alisema Bi. Mwajuma
Tanzania imeshiriki katika Mkutano wa Tatu wa Wanawake nchini Urusi uliofanyika nchini humo kuanzia tarehe 13-15 Oktoba 2021 ambapo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt Dorothy Gwajima alimwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan.
Mkurugenzi
wa Idara ya Maendeleo ya Jinsia kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) Mwajuma
Magwiza akishiriki katika moja ya mkutano katika Mkutano wa tatu wa
Wanawake nchini Urusi uliofanyika Oktoba 13-15 jijini Saint Petersburg.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...