Na Karama Kenyunko Michuzi TV
TUME ya vyuo Vikuu Tanzania(TCU), imefungua dirisha la udahili kwa awamu ya nne kwa mwaka wa masomo 2021/2022 dirisha ambalo litaanza Oktoba 11 hadi Oktoba 15 mwaka huu 2021.

Hatua hiyo imekuja baada ya kukamilika kwa udahili wa awamu tatu na kuonekana kuna baadhi ya wanafunzi hawakuweza kukamilisha ufadhili wao katika dirisha la kwanza hadi la tatu ukizingatia wakati huu ambao Taasisi za Elimu ya juu nchini zinasema kuwa kuna nafasi katika baadhi ya masomo kwa mwaka huu wa masomo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Oktoba 11,2021 Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Charles Kihampa amesema lengo ni kutoa fursa kwa waombaji ambao hawakuweza kuomba udahili katika awamu tatu zilizopita kutokana na sababu mbalimbali.

"Tume imepokea maombi ya kuongezea muda wa udahili kutoka kwa baadhi ya wa waombaji na Taasisi za Elimu ya Juu nchini ambazo bado zina nafasi katika baadhi ya Programu za masomo kwa mwaka 2021/2022

Aidha Tume imevitaka vyuo kuhakikisha Program ambazo watafungua katika dirisha hili ni zile zenye nafasi tu huku zile ambazo zinejaa wakitakiwa kuendelea Kuzifunga ili kuepusha changamoto ambazo zinaweza Kujitokeza Hapo baadae.

“Kama tume pia tunasisitiza vyuo vyote kuzingatia idadi ya wanafunzi iliyoidhinishwa katika programu husika na kwa waombaji wote wanakumbushwa masuala yote yanayohusiana na udahili ama kujithibitisha yawasilishwe moja kwa moja kwenye vyuo na siyo TCU,” amesema Profesa Kihampa.

Amewakumbusha waombaji wote kuwa masuala ya yanayohusiana na udahiliama kuthibitisha yawasilishwe moja kwa moja katika vyuo husika na si TCU.

Pia Profesa Kimpa amesema zoezi la uhakiki wanafunzi kwa wale ambao walidahiliwa kwenye chuo zaidi ya kimoja linaendelea ambapo linatarajiwa kukamilika Octoba 24.
Katibu Mtendaji wa tume ya vyuo Vikuu Tanzania(TCU), Prof. Charles Kihampa akizingumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati akitangaza kufunguliwa kwa dirisha la nne la udahili jijini Dar es Salaam.

Katibu Mtendaji wa tume ya vyuo Vikuu Tanzania(TCU)Prof. Charles Kihampa (katikati) akizumza na waandishi wa habari (hawamo pichani) wakati wa mkutano huo uliofanyika kwenye Ofisi za Tume hiyo Jijini Dar es Salaam. (wa kwanza kulia) ni Mkurugenzi wa uratibu wa Udahili na utunzaji wa Kanzidata wa Time hiyo Dkt Kokuberwa Kulunzi-mollel, na (kushoto) ni Kaimu Mkurugenzi wa huduma za Taasisi (TCU) Bwa. Yusuf Rauna.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...