Ubalozi wa Tanzania nchini Namibia umeandaa maonyesho ya biashara yanayofanyika kuanzia tarehe 4 hadi 8 Oktoba, 2021 katika Kituo cha Biashara cha Wernhil (Wernhil Shopping Mall) kilichopo mjini Windhoek. Maonesho haya muhimu katika utelezaji wa Diplomasia ya Uchumi yanalenga kutangaza bidhaa za Tanzania na Utalii nchini humo ili kukuza biashara na kuvutia wawekezaji nchini.
Katika maonesho hayo Ubalozi umewashirikisha Watanzania wajisiriamali na wafanyabiashara waishio nchini humo (diaspora) ambao wamejitokeza kuonesha bidhaa mbalimbali ikiwemo mchele, korosho, kahawa, asali, majani ya chai, maharagwe, vitenge, batiki na nguo za kufuma.
Sambamba na kunesha bidhaa maonyesho haya yamejumuisha uuzaji wa vyakula mbalimbali vya kitanzania ambavyo vimekuwa vivutio kwa wateja wengi.
Maonesho hayo yalifunguliwa na Balozi wa Tanzania nchini Namibia Mhe. Dkt. Modestus Kipilimba tarehe 4 Oktoba 2020.
Balozi wa Tanzania nchini Namibia Mhe. Dkt. Modestus Kipilimba akiwasili katika Kituo cha Biashara cha Wernhil (Wernhil Shopping Mall) kilichopo mjini Windhoek, Namibia kwa ajili ya ufunguzi wa maonesho ya biashara.
Balozi
wa Tanzania nchini Namibia Mhe. Dkt. Modestus Kipilimba akitazama
sehemu ya bidhaa za Kitanzania kwenye maonesho yanayoendelea katika
Kituo cha Biashara cha Wernhil Shopping Mall mjini Windhoek, Nambia.
Balozi
wa Tanzania nchini Namibia Mhe. Dkt. Modestus Kipilimba akiwa katika
picha ya pamoja na baadhi ya Wafanyabiashara wa Kitanzania waliojitokeza
kuonesha bidhaa zao kwenye maonesho yanayoendelea katika Kituo cha
Biashara cha Wernhil Shopping Mall mjini Windhoek, Namibia.
Sehemu ya wafanyabiashara wa Kitanzania wakionesha bidhaa zao kwenye
maonesho yanayoendelea katika Kituo cha Biashara cha Wernhil Shopping
Mall mjini Windhoek, Namibia.
Balozi
wa Tanzania nchini Namibia Mhe. Dkt. Modestus Kipilimba akiwa katika
picha ya pamoja na Maafisa wa Ubalozi huo walipotembele maonesho ya
Biashara yanayoendelea katika Kituo cha Biashara cha Wernhil Shopping
Mall mjini Windhoek, Namibia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...