Na Mwamvua Mwinyi, Mkuranga
MBUNGE
wa Jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega amewahakikishia wakazi wa
KondoMwelanzi kata ya Bupu kupata kipaombele Cha kujengewa daraja la mto
Kipilimba ili kuondoa kero wanayoipata wakati wa mvua kushindwa
kupitika.
Aidha mbunge
huyo ameielekeza wakala wa barabara Vijijini (TARURA )wilaya ya Mkuranga
kuzipa kipaombele barabara kero Kibudi- Mbulani pamoja na Panzuo shule
ambapo wakazi wa Kibudi hulazimika kutumia usafiri wa pikipiki kwenda na
kurudi sh.10,000.
Ulega
alibainisha hayo katika ziara yake ya Jimbo kata ya Panzuo na Bupu
kwenye vijiji vya Mbulani,Tundu,Kibudi,na Kondo Mwelanzi ambapo aliitaka
TARURA kuweka ujenzi wa daraja hilo katika bajeti ijayo 2022-2023.
Alieleza
,imeshatolewa milioni 100 kwaajili ya maboresho barabara kuu ya Bupu
-Kiparanganda sasa TARURA ifungue na barabara Tundu-Kiziko ,Bupu-Kibudi
,Zogowale kuondoa eneo korofi,ili kuleta maendeleo kwa wananchi.
Ulega aliielekeza pia TANESCO
kufikisha
umeme Mbulani-Panzuo kwa wateja walikwishalipia ,zahanati ya
Panzuo,sekondari Panzuo,na Shule ya sek Mandikongo na Shule ya msingi
Mamrimpera.
Aliwaeleza wananchi wa kata hizo kuvuta subira kwa changamoto ambazo bado zipo kwenye mchakato wa kutatuliwa.
"Serikali
ya awamu ya sita inapiga kazi katika sekta zote ,na hadi sasa mh.Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan ameshatoa tilioni
1.3 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 15,000 nchi nzima,
"Serikali pia imetenga kiasi cha sh.bilioni 966 kwa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) ili kuboresha barabara pamoja na madaraja maeneo mbalimbali nchini"Yaani Samia anaupiga mwingi ile mbaya ,tumpe ushirikiano na tuendelee kumuamini na kumuunga mkono"alisisitiza Ulega.
Katika
ziara hiyo Ulega ametoa mifuko ya saruji 50 na sh.500,000 katika ujenzi
wa zahanati Kibudi na pamoja na mifuko ya saruji 50 na sh .500,000 Bupu
ujenzi wa zahanati ,500,000 ujenzi wa msikiti ,Tundu ujenzi wa nyumba
ya mganga 500,000 na mifuko ya saruji 50,Mbulani mifuko ya saruji 50 na
sh .400,000 kwa ajili ya wodi ya wazazi zahanati ya Mbulani na
amechangia baadhi ya vikundi vya akinamama ikiwa ni fedha sh 800,000
fedha zake binafsi.
Awali
diwani wa kata ya Panzuo Dude Hamis alisema, wanakabiliwa na changamoto
ya umeme ambapo nyumba zilizokadiria zilikuwa 125 zilizopata ni 20
pekee licha ya wateja hao kulipia toka Juni mwaka huu huku zahanati
wakitumia tochi na vibatari.
Jingine
ni shule ya msingi ni ya muda mrefu imejengwa miaka ya 70 ,hawajapata
madarasa na yaliyopo ni chakavu , barabara ya Zogowale ni eneo korofi
eneo la mlima linahitajika kujengwa mitalo .
Meneja wa TARURA Mkuranga Silas alisema tayari kiasi Cha sh .milioni 120 kipo kwa ajili ya bajeti hii .
Akijibu kuhusiana na ombi la ujenzi wa daraja Dondwe-mto Kipilimba alisema amelipokea na watalipa kipaombele bajeti ijayo .
Nae
meneja wa TANESCO Mkuranga Theodory Hall alisema ,baada ya wiki mbili
wataanza na zoezi la kuunganishia wale waliolipia Mbulani na kudai
baadhi ya maeneo yapo kwenye mpango wa REA na kuwahakikishia umeme
kwenye utafika katika maeneo aliyoomba mbunge Ulega ikiwemo shule za
sekondari ,msingi na zahanati .
Mwenyekiti
wa CCM Mkuranga,Ally Msikamo aliwataka wataalamu watoke maofisini na
kwenda maeneo ya Vijijini kujionea uhalisia wa changamoto zinagusa
wananchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...